Jumatatu, 4 Januari 2016

UKUAJI WA THAMANI YA HISA DSE YAONGEZA IDADI YAMAUZO YA HISA JIJINI.


Timothy Marko .

WASTANI Wa bei ya mauzo yahisa katika kipindi cha mwaka  2014-2015 umeweza kufikia shilingili bilioni 50ikilinganishwa nakipindi cha mwaka 2011 ambapo zaidi ya shilingi bilioni252 ziliweza kuwekekezwa katika soko la hisa la Dar es salaam (DSE).

Meneja Fedha soko la Hisa Dar es salaam DSE IBRAHIMU MSHINDO akitoa ufafanuzi kuhusiana namwenendo wa soko la mitaji katika soko la hisa Dares salaam mapema hii leo

Akizungumza na waandishi wa Habari Meneja Fedha wa soko hilo Ibrahimu Mshindo amesemakuwa wastani wamauzo hayo yahisa kumetokana na kuongezeka kwa thamani ya mauzo ya hisa za makampuni zinazo uzwa na soko hilo la mitaji .

‘’KATIKA kipindi cha Mwaka 2012hadi mwaka jana wastani wa dhamana iliweza kufikia shilingi bilioni 5O ikilinganishwa nakipindi cha mwaka 2011 ambapo wastani shilingi bilioni252 ziliweza kuwekezwa ‘’Alisema Meneja Fedha Ibrahimu Mshindo. .

Meneja MSHINDO alisema kuwa katika kipindi cha mwaka 2014 zaidi shilingi bilioni 2,382 ziliweza kuwekezwa  ambapo  jumla shilingi trioni moja ziliweza kuwekezwa katika kipindi cha mwaka jana .

Alisema kuwa ongezeko hilo nizaidi yamara nne ambapo zaidi shilingi bilioni 50ziliweza kuwekezwa katika kipindi cha mwaka 2011ambapo zaidi yashilingi trionimoja ziliweza kupatikana katika kipindi cha mwaka jana .

‘’Ongezeko hili limechangiwa na baadhi yamakampuni kuongezeka nakukuza ufaninisi wa makampuni hayo katika soko baada ya makampuni kuongeza ubora wake kwa kutumia tekinolojia  katika kupunguza muda wakutoa huduma ‘’Aliongeza Mshindo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni