Alhamisi, 31 Desemba 2015

SOKO LAHISA LAFUNGA MWAKA KWAKUZA ZA SHILINGI TRIONI MOJA 2015



Timothy Marko.
KIWANGO cha Uuzwaji wa hisa katika soko lahisa la Dar es salaam (DSE)kimeongezeka kutoka shilingi bilioni 13 .8 nakufikia shilingi trioni moja kwakipindi cha  mwezi January Hadi DESEMBA mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wahabari jijini Meneja Mauzo na naBiashara wa soko la hisa la Dar es salaam DSE Patrick Mususa amesema kuwa ongezeko hilo limetokana na kuwepo kwa ongezeko la hati fungani pamoja na muamuko mkubwa kwa wa wawekezaji kununua hisa katika soko hilo .
‘’Ongezeko hili la ununuzi wahisa limetokana na ongezeko la hati fungani nakuwepo kwa mwamuko mkubwa kwa baadhi ya wananchi kununua hisa zilizo katika soko hilo la hisa ‘’Alisema Patrick Mususa .
Meneja Mauzo Mususa alisema kuwa kuwepo kwa ongezeko lafaida katika hisa zinazo uzwa nasoko hilo kumeweza kuongeza manunuzi yahisa hali inayochangiwa namwamuko wa ununuzi wa hisa .
Alisema kuwa zaidi yawawekezaji watapatao 200000 wamewez a kujinga nasoko hilo nakuorodheshwa hali inayochangiwa na taasisi hiyo kutumia mbinu zakisasa ikiwemo za mifumo ya komputa pamoja nasimu kuuza hiza zake .
‘’Tunavyoingia mwaka mpya kuna teknolojia mpya ikiwemo Smart Phone ilikuweza kujiunga nahuduma zinazotolewa na nasoko la hisa ‘’Aliongeza Meneja Mauzo MUSUSA .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni