Ijumaa, 22 Januari 2016

AFISA AFYA AWATAKA WATENDAJI WA SERIKALI ZA MITAA KUDUMUMISHA USAFI JIJINI DAR ES SALAAM.



Timothy Marko.
KATIKA kuhakikisha afya za wananchi wa mkoa wa Dar es salaam zinaimarika nakuondokana natatizo la kipindu pindu ,Afisa afya mkoa huo amewataka watendaji wa ngazi ya wilaya zote kuweza kuboresha hali ya vitendea kazi ilkuweza kuboresha hali ya usafi .

Akizungumza katika mkutano wa watendaji wa manispaazote  , mkoa Dar es salaam Afisa afya Bakari Mhina amesema  kuwa nivyema serikali ikaunda idara ya mazingira itakayo simamia masuala ya usafi katika kata zote katika mkoa huo .

‘’Tunaiomba serikali iweze kuandaa idara yausafi na mazingira ambayo itaainisha majukumu ya idara hii kwani hali yausafi sio ya kuridhisha katika mkoa wetu ‘’Alisema Afisa afya BAKARI MHINA.
Afisa afya MHINA alisema kuwa uundwaji wa idara hiyo kutwezesha kuimarisha hali yausafi katika kata zote za mkoa wa Dar es salaam .

Alisema kuwa pamoja na kuzitaka manispaa hizo kudumisha hali ya usafi katika mkoa wa Dar es salam pia ameongeza kuwa atazitafutia ufumbuzi wa changamoto za vitendea kazi ikiwemo rasmali fedha katika kudumisha usafi .

‘’Nafahamu changamoto mlizonazo katika kutekeleza suala hili linahitaji vifaa na rasmali fedha nitawasilisha mapendekezo yenu katika serikali kuu ilikuweza kutatua changamoto hizi ‘’Aliongeza MHINA.

Afisa  afya wilaya ya Temeke Irene Chuwa alizitaja changamoto zilizopo katika wilayayake kuwa wilaya hiyo inakabiliwa natatizo lauchafu hali inayotokana nakuwepo kwa wakandarasi wachache wakufanya shughuli hiyo .

Alisema kuwa sambamba nauhaba wa wakandarasi pia wiaya hiyo inakabiliwa na uhaba wa vitendea kazi ili kufanikisha suala zima la usafi .

‘’Katika wilaya yetu ndugu mwenyekiti tunakbiliwa na changamoto ya uhaba wa wakandarasi wa kuzoa taka na uhaba wa vifaa vyakufanyia usafi ‘’Alisema IRENE CHUWA.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni