Timothy
Marko.
KATIKA
kuhakikisha sekta ya Habari nchini inaendana nakasi ya sayansi na teknolojia serikali
ya Tanzania imeingia makubaliano yakubadilishana uzoefu na nchi ya china .
Akizungumza
katika mkutano wa makubaliano hayo jijini Dar es salaam mapema hii leo Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Elisante ole Gabriel amesema kuwa kutokana na nchi hiyo
kukua kwa kasi katika Nyanja ya tekinolojia na mawasiliano hivyo nifursa nzuri
kwa nchi ya Tanzania kubadilishana uzoefu wa kitekenolojia ili kuwezesha sekta
ya habari kukua .
‘’Eneo la
Tekinolojia china imekuwa ikikuwa kwa kasi hivyo kama sisi serikali ya Tanzania
tumeona nifursa nzuri kwa watalamu na wadau wetu wa habari kuja china
nawatalamu wenu kuja hapa Tanzania ili kubadilishana uzoefu katika eneo hili ‘’Alisema
Katibu Mkuu ELisante ole Gabriel.
Katibu Mkuu
Elisante alisema kuwa sambamba nchi yachina kukuwa katika eneo la teknolojia
pia serikali ya Tanzania imeonelea nifursa muhimu kubadilishana watalamu
mbalimbali wa lugha yakiswahili na kichina ilikuweza kuukuza lugha hizo mbili
kwa manufaa yanchi hizo .
Alisema
serikali ya Tanzania ipotayari katika kuwaruhusu wa talamu wasekta ya habari wa
vyombo vya habari vya Televisheni na Magazeti kuweza kupataziara ya mafunzo
yakukuza uzoefu katika tasnia hiyo .
‘’Tungependa
serikali ya china na serikali ya Tanzania
kuweza kubadilishana uzoefu baina yanchi zote mbili katika sekta ya
habari hususan watalamu wetu habari wamagazeti pamoja Televisheni kuweza kupata
ziara yakimafunzo ili kuweza kubadilishana uzoefu nchini china ‘’Aliongeza
Katibu Mkuu ELISANTE .
WAZIRI wa
habari wa china TIAN JIN amesema kuwa serikali ya nchi hiyo ipotayari kukuza
ushirikiano nanchi ya Tanzania katika sekta ya habari kwa kuwakaribisha wadau
wasekta hiyo kuhudhuria mkutano wakimataifa wa vyombo vya habari kutoka afrika
na china utakaofanyika hivi karibuni .
Alisema kuwa
katika mkutano huo vyombo vyautangazaji vya Televisheni na magazeti ya serikali
vinakaribishwa kuhudhuduria mkutano huo .
‘’Tunao
mkutano wa wadau wa habari kutoka Barani afrika pamoja na china kuweza
khudhuria mkutano huu wa wadau wa vyombo vya habari ‘’Alisema Tian Jin.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni