Timothy Marko.
TANZANIA
imekuwa nchi ya 82 kati yanchi 100 duniani zenye mazingira huru yakiuchumi kwakipindi cha mwaka huu ikilinganishwa
nafasi92 mwaka jana kwamujibu wa ripoti ya uhuru wa uchumi wa Dunia(Economic Freedom of the world
Repot) .
Ripoti hiyo
imetolewa na Mkurugezi mtendaji wa taasisi ya Uhuru Intiative Policy Education Isack
Danford ambapo amesema kuwa vigezo vilivyoweza kuiwezesha nchi ya Tanzania
Kushika nafasi hiyo nikutokana na kuwepo kwa mifumo ya udhibiti wa bishara za
ndani ,kudhibiti vitendo vya hongo,upendeleo wa utoaji huduma kwa umma na
gharama za huduma katika ofisi za umma zinazotokana na urasimu.
‘’Masuala
mengine yaliyoweza kuifikisha Tanzania katika nafasi ya 82 nipamoja na kuwepo
kwa mahitaji yakiutawala ,ulazimishaji wa kuchangia huduma za kiserikali pamoja
na makubaliano ya Mishahara ‘’Alisema Isack Danford .
Mkurugenzi
Danford alisema kuwa viwango vingine vilivyopelekea Tanzania kushika nafasi hiyo nipamoja na
kuwepo kwa vikwazo katika uwekezaji ambavyo visivyo vya kiforodha nakuwepo kwa
utofauti wautowaji waviwango vya forodha .
Alisema kuwa
sambamba naviwango hivyo kupungua kwa thamani shilingi ya Tanzania katika soko
ladunia imechangia Tanzania kushika nafasihiyo ya 82 ikilinganishwa na nchi za
afrika mashariki .
‘’Nchi
nyingine zilizo kuwa katika ukanda wa afrika mashariki nipamoja na Kenya ikishika
nafasi ya sitini ambayo ilikuwa nikinara katika uchumi katika ukanda wa afrika
mashariki ,wakati Ruwanda ambayo sasa
inashika nafasi yakwanza katika afrika mashariki inashika nafasi thelathini na
nne na Uganda inashika nafasi yamwisho katika nchi za ukanda wa afrika
mashariki ikishika nafasi ya arobani duniani ‘’Aliongeza Isack Danford .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni