Blogu hii makini iko kwa ajili ya kuhabarisha masuala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Karibuni sana.
Alhamisi, 19 Novemba 2015
KAMPUNI YA SBC TANZANIA LTM YAPUNGUZA BEI ZA VINYWAJI VYAKE.
Timothy Marko .
KATIKA kuhakikisha maisha yawatanzania yanaboreshwa kiuchumi kampuni ya SBC Tanzania Limited kupitia kinywaji cha pepsi nchini Imeshusha kiwango cha bei za bidhaa zake ilikuwawezesha wateja wake kuweza kupata huduma zake .
Akizungumza na waandishi wa Habari mapema hii leo jijini Dar es salaam Meneja Mauzo wa Kampuni ya SBC Tanzania limited Rashid Chenja amesema kuwa kampuni hiyo imeamua kushusha bidhaa zake ikiwemo soda zinazo zalishwa katika kiwanda hicho kutoka shilingi 600 hadi kufikia shilingi 500.
‘’Tumeamua kupunguza bei ya bidhaa zetu ikiwemo soda zinazozalishwa nakampuni yetu ya SBC Tanzania ikiwemo soda za pepsi cola ,seven up ,Everest ,Mountdew ,pamoja na mirinda kutoka shilingi 600 hadi 500 Hali hii imetokana na ugumu wa maisha wa wateja wetu ‘’Alisema Meneja Mauzo Rashid Chenja .
Menja Mauzo Rashidi Chenja alisema kuwa maeneo yatakayo husika na punguzo hilo nipamoja na mikoa ya Dar es salaam,Morogoro ,Tanga, pwani ,Lindi ,pamoja Zanzibar .
‘’Tuliwezaku kusanya maoni ya wadau wetu kuhusiana na punguzo la bei yabidhaa zetu ambapo punguzo hili limeanza tangu tarehe 16Novembar mwaka huu ‘’Aliongeza Meneja Mauzo wa kampuni ya SBC Tanzania limited .
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni