Blogu hii makini iko kwa ajili ya kuhabarisha masuala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Karibuni sana.
Ijumaa, 20 Novemba 2015
SERIKALI:TUNAENENDEA KUIPITIA SERA YA MTOTO ILI IWE SHERIA .
Timothy Marko.
SERIKALI imesema kuwa inaendelea kuweka mipango mbalimbali ya kuratibu sera kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo wa jumuhia ya ulaya katika kutokomeza tatizo la ukatili dhidi ya watoto .
Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya watoto duniani yaliyofanyika jijini Dar es salaam mapema hii leo ,Kaimu Kamishina msaidizi wa maendeleo ya mtoto kutoka wizara afya na ustawi wajamii Danieli Masunza amesema kuwa kutokana na mipango hiyo ikiwemo kupitia vifungu vya sheria ya mtoto ya mwaka 2009 pamoja na ile ya mwaka 2011ili kuweza kutatua changamoto zinazo mkabili mtoto ikiwemo ndoa za utotoni .
‘’Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika kupambana na tatizo la ukatili dhidi ya watoto kwa kupitia vifungu mbalimbali vya sheria ya mtoto ya mwaka 2009,na ile ya mwaka 2011’’Alisema Kaimu Kamishina Danieli Masuza .
Kaimu Kamishina Masuza alisema kuwa jumla yawilaya 33zimetengwa katika utekelezwaji wamiradi mbali mbali yakutokomeza tatizo la ukatili dhidi ya watoto .
Alisema kuwa zoezi hilo litajumuisha katika kuanzisha tafiti mbalimbali dhidi ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu kwa kushirikiana nataasisi za kiserikali ikiwemo vyombo vya dola ikiwemo polisi .
‘’Miradi hii itajumuhisha katika wilaya za kisarawe,kibaha ambapo vipaumbale katika utekelezaji wamipango hiyo itazingatia sera ya mwaka 2009/2010 ya mtoto ‘’Aliongeza Kaimu kamishina Danieli Masuza .
Katika hatua nyingine Muwakilishi mkaazi wa shirika la watoto la umoja wa mataifa UNICEF Georgina Mtenga amesema kuwa katika utafiti uliofanywa nashirika hilo limebaini kuwa jamii nyingi za kitanzania zimekuwa zikitoa adhabu ya viboko kwa watoto ikiwa ni njia ya kumrekebisha mtoto ,hata hivyo shirika hilo limesema utamaduni wa viboko kwa watoto ni ukatili wa kijinsia kwa watoto hao.
Georgina MTENGA alisema kuwa sambamba na utoaji adhabu ya viboko kwa watoto hao bado pia kumekuwepo nachangamoto za ndoa za utotoni .
‘’Adhabu ya watoto ikiwemo viboko imekuwa niutamaduni wa jamii za kitanzania ambapo pia vitabu vya dini hususa dini ya kikisto umekuwa ikiruhusu uchapaji viboko ambao ni ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto.’’ Alisema Mtenga .
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni