Jumatano, 1 Machi 2017

BANDARI YA DAR ES SALAAM YAZINDUA MASHINE YAUKAGUZI WAMIZIGO .

Timothy Marko.
 Katika kuhahikisha sekta ya bandari inakuwa nakujenga uchumi katika nchi ya Tanzania JUMLA ya shilingi bilioni 20.28 zimetumika Kukarabati Mradi wa Scana uliopo katika Bandari ya Dar es salaam pamoja na Tanga .

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari jijini Dar es Salaam Mhandisi Deus Kakoko wakati wauzinduzi wa mashine yaukaguzi mzigo bandarini hapo ambapo amesema kuwa uzinduzi wa Scana hiyo imetokana namsaada kutoka Jamuhuri ya watu wachina ili kuweza kukuza sekta ya bandari nchini .

''Scana hizi ambazo zimegharimu shilingi bilioni20.28 sambamba na Magari yaukaguzi wa bidhaa zinzoletwa bandarini umetokana na makubaliano yanchi mbili kati yachina na Tanzania ikiwa nijuhudi za nchi hizo kukuza sekta ya bandari sio Dar es salaam tu bali katika ukandakusini mwaafrika ambapo bidhaa nyingi hupita bandari ya Dar es salaam''Alisema Mkurugenzi Deusi Kakoko .

Mkurugenzi kakoko amesema upatikanaji wascana hizo katika bandari kutaweza kurahisisha zoezi lauhakiki kwa kipindi kifupi ambapo bidhaa moja itahakikiwa kwa saa moja nakupukana upotevu wamapato ya serikali yatokanayo nakodi .
Alisema Mradi huo utakuwa mwarobaini kwa wafanyabishara wanaohifadhi bidhaa zao katika bandari hiyo pasipo kulipa kodi stahiki yaushuru wa bidhaa bandarini hapo .
''Scana hizi zitasaidia ukwepaji wakodi nakuweza kutokomeza biashara haramu ya magendo ''Aliongeza KAKOKO.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni