Alhamisi, 23 Februari 2017

MAKONDA AWATAKA WANANCHI KUCHANGAMKIA FURSA UJIO WA RAIS MSEVENI.

Tokeo la picha la paul makonda
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaamPaul Makonda

Timothy Marko.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaamPaul Makonda  amewataka waakazi wa jiji la Dar es Salaam Kujitokeza katika kuwakaribisha Marais wawili kutoka uganda na visiwa vya shelisheli wanaotarajiwa kufika jijini Dar es salaam Febuari 25 hadi  27 Mwaka huu.

Akizunguza juu yaujio wa Marais wa Visiwa vya Shelisheli  Danny Faure na Yoweri Kaguta Mseveni wa nchini Uganda jijini Dar es salaam paul Makonda amesema kuwa wageni hao watakuja nchini Tanzania  
wakiwa na ajenda yakukuza uhusiano wakiuchumi na biashara kati yanchi hizo na Tanzania .
''Ujio huu Wa Marais hawa wawili unaonesha juuhudi kubwa ya Rais wa Awamu ya Tano Wa Tanzania Dk.Jonh Pombe Magufuli katika kukuza siasa za kimataifa ''Alisema Mkuu wa Mkoa Paul Makonda .

Makonda amesema kuwa ujio wamarais hao wawili nifursa muhimu kaika kukuza uchumi kwani wanatarajia marais hao kuweza kutembelea vivutio vya utalii vilivyomo kaika visiwa vyazanzibar kama nyanja yakukuza diplomasia yaikuchumi nchini .
Alisema Nilazima Wajasriamali wakitanzania kuweza kutumia fursa hiyo kama nyanja yakukuza biashara katika nchi hizo kwakuweza kutng'eneza bidhaa zitakazo kuza bashara baina yanchi hizo .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni