Jumatatu, 28 Novemba 2016

WABUNGE KUSHIRIKI MASHINDANO NCHINI KENYA .

Tokeo la picha la wabunge wa tanzania
BAADHI YA WABUNGE WAJAMUHURI WA MUUNGANO WA TANZANIA
Timothy Marko
Timu ya Wabunge inatarajiwa kushiriki ligi ya Wabunge wa afrika Mashariki Desember 4 mwaka huu huko Nairobi Nchini Kenya .

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mwenyekiti  Wa timu ya  Bunge  William Ngeleja jijini Dar es salaam  amesema kuwa Timu hiyo inatarajiwa kushiriki Mashindano hayo kutokana na Mkataba wa jumuhia hiyo unaolenga kuimarisha uhusiano baina ya nchi wanachama wajumuihia ya Afrika Mashariki .

''Nchi ambazo zinatarajiwa kushiriki mashindano haya nipamoja Tanzania ,Kenya ,uganda Ruwanda sudani kusini pamoja na Burundi ambapo michezo mbalimbali inatarajiwa kuchezwa ikiwemo Mchezo wasoka ,pete ,wavu Vollabe riadha pamoja nakuvuta kamba '''Alisema Mwenyekiti wa Timu ya wabunge William Ngeleja .

Ngeleja alisema kuwa Msafara wa timu hiyo utakuwa niwatu sitini ambapo utajumuisha wachezaji mbalimbali wa ngazi tofauti ikiwemo mpira wamiguu ,kuvuta kamba ,mpira wapete vollable ,pamoja na mpira wapete .

Alisema kila kikosi kitaongozwa na manahodha ambapo kikosi cha vollable ikitaongozwa na Mheshimiwa Saumu SAKALA,kikosi  champira wapete Kitaongozwa na Mheshimiwa Grace Kiwelu ,kikosi cha kuvuta kamba kitaongozwa na Anna lupembe wakati Mpira wamiguu Kikosi kitaongozwa Hamidu bobali.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni