HASSAN SILAYO-MAELEZO
Zoezi la uhakiki wa watumishi wa umma linaloendelea kwa sasa litasaidia kuja na orodha sahihi ya watumishi halali wa umma na kupunguza kabisa idadi ya watumishi hewa serikalini.
akiongea
katika kipindi cha TUNATEKELEZA kinachoratibiwa na Idara ya
Habari(MAELEZO) kwa ushirikiano na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora Dkt. Laurean Ndumbaro amesema kuwa zoezi hili limekuwa na mafanikio
makubwa kwani litasaidia kubaini watumishi hewa na kuwatoa katika mfumo
wa ajira kutokana na kuiingizia serikali hasara.
"Zoezi
hili tunaloliratibu kwa sasa kwa ushirikiano na NIDA litasaidia
kuwaondoa watumishi hewa serikalini ambao kwa takwimu imeonesha serikali
ilikuwa ikilipa mabilioni ya fedha kwa waajiriwa hewa kutokana na
kutokuwa na taarifa sahihi za watumishi wa serikali jambo ambalo
litakoma siku chache zijazo kwa uwepo wa orodha sahihi ya watumishi wa
umma" Alisema Dkt. Ndumbaro.
Dkt. Ndumbaro
alisema kuwa baada ya kuliendesha kwa mafanikio zoezi hili linatarajiwa
kumalizika ndani ya mwezi huu hivyo kuziwezesha taasisi za serikali kuwa
na orodha sahihi ya watumishi wa umma hivyo zoezi la kuajiri
litaendelea kama kawaida pia kuwaingiza katika mfumo waajiriwa wapya
ambao ajira zao zilisitishwa kwa muda.
Aidha
Dkt. Ndumbaro alisema kuwa baada ya zoezi hili serikali itajaza nafasi
zote zilizowazi baada ya watumishi hewa kuondolewa katika mfumo wa ajira
serikalini
Wakati
Huohuo Dkt. Ndumbaro amesema kuwa upandishaji vyeo kwa watumishi wote
wa umma utazingatia utendaji kazi wa mhusika katika eneo lake na kazi.
Naye
Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bi. Suzan Mlay amewataka viongozi wa
serikali kutumia lugha nzuri kwa waliochini yao ikiwamo kufuata kanuni
sheria na taratibu za kiutumishi katika kutekeleza majukumu yao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni