Waziri wa Maliasili na utalii Profesa Jumanne
Magembe akizungumza na baadhi ya
watendaji na wafanyakazi wa chuo cha utalii nchini (hawapo pichani)
|
Timothy mark
Waziri wa maliasili na
Utalii nchini Prof. Jumanne Magembe amewataka watendaji wa chuo cha utalii cha
Taifa kuweza kukiendesha kwa faida na kutokutegemea ruzuku kutoka serikali kuu.
Akizungumza katika
ziara ya kutembelea moja ya idara anazozisimamia katika wizara yake Prof.
Magembe amesema, ni vema chuo hicho kiweze kuboresha mitaala yake ikiwa ni
pamoja na kuendana soko la utalii nchini, kwani sekta hiyo imekuwa ni kitovu
kikubwa cha uchumi na mapato kwa taifa.
Hata hivyo Prof.
Magembe amesema kuwa ni ajabu kuona baadhi ya hoteli nchini zenye nyota tano
zikiwa hazina wafanyakazi wazalendo wa kitanzania badala yake wanachukua
wafanyakazi kutoka nje ya nchi, pia amesikitishwa na kitendo cha chuo hicho
kutokuwa na mazingira yasiyoridhisha ingawa wana kila kitu kinachotakiwa
kufanyika kuwa cha kisasa.
Aidha waziri Magembe
ameshangazwa na kitendo cha bodi hiyo kutothamini sekta ya utalii ambayo
imeonekana kutoa ajira kwa watanzania zaidi ya 500,000 huku walio nje na walio
jiajili wenyewe kuwadumia watalii ni 1,200,000 hata hivyo amesisitiza kuwa
sekta hiyo kiini chake kipo kwenye katika sekta binafsi.
Katika hatua nyingine
Waziri Magembe amewataadhalisha watendaji wa chuo hicho kujitathimini kwa
kutoigemea serikali kwa kuililia kupewa ruzuku na kuwafananisha sawa na machungwa
yaliyowekwa mahala pasipokuwa pa kwake.
Wakati huohuo amekitaka
chuo hicho kutobadiri malengo yake ya kutoa wataalam na badala yake waache mara
moja kujifanya kuwa wakala wa sekta ya utalii na mahoteli nchini. “Kuanzia sasa
hiki chuo siyo wakala ni chuo cha Utalii cha Taifa.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni