Timothy Marko.
Mahakama Kuu ya Tanzania Kitengo Cha Ardhi imetupilia mbali shauri la Freeman Mbowe dhidi ya kampuni yake ya Free media Group na Shirika la Nyumba nchini (NHC) kutokana nakile kinachoitwa kuwepo kwa mapungufu ya sheria ya mkataba dhidi ya shirika lanyumba nchini .
Kwamujibu wa jaji wa Mahakama hiyo sivangilwa Mwangosi aliyesikiliza maamuzi ya pande mbili kati ya Shirika lanyumba na Free media Group ulibanisha kuwa katika upande washirika lanyumba wakili wa shirikahilo Aliko Mwamanenge alidai kuwa baadhi ya mashauri yalipo katika shauri hilo hayakuweza kufwatwa kama utaratibu wa kimahakama unavyo elekeza .
''kutokana baadhi ya taratibu kutoweza kufwatwa hii inaonesha wazi tumimenyimwa haki lakini hadi sasa tunaidai Free MEDIA Shilingi bilioni 1.17 kutokana na kutofwatwa kwa taratibu za kisheria NHC imeshinda ila kesi yamsingi tumeshinda ''Alisema MWAMANENGE .
Kwaupande wake kampuni ya Freemedia Group imedai kuwa kampuni hiyo imeupokea uamuzi ulkliotolewa namahakama ,lakini kampuni hiyo ilidai kuwa inatarajia kufungua kesi nyingine .
Wakili wa mbowe jonh Malya aliitaka mahakama kuweza kumpa muda wa kupitia maamuzi yaliyotolewa na mahakama hiyo ilkuweza kutoa maamuzi sahihi .
''Tuanaanza nakuiomba mahakama iweze kutupanakala ya uamuzi ambapo jambo hilo lina anza leo ili kuweza kukata rufaa ''Alisema Malya .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni