Timothy
Marko.
SERIKALI
imewataka wahisani mbali mbali kuweza kutoa michango mbalimbali ilikuweza
kuwasaidia wahanga watetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera hivi karibuni
.
Akizungumza
katika ufunguzi wa kongamano la uwezeshaji wa mifuko ya jamii jijini Dar es
salaam Katibu Mkuu ofisi ya Rais Peter ilomo amesema hadi hivi sasa tetemeko
hilo watu ishirini wamepoteza maisha yao
,huku jumla ya nyumba takribani 7840 zimeweza kuharibiwa natetemeko hilo .
‘’Ninaziomba
taasisi najumuhia mbalimbali za kimataifa kuweza kutuchangia kupitia mfuko wa
majanga ilikuweza kufanya marekebisho ya sehemu zilizo haribiwa ‘’Alisema
Katibu Mkuu Peter Ilomo .
Katibu Mkuu
ofisi ya Rais Ilomo amesema kuwa kupitia mfuko huo wa majanga serikali itaweza
kufanyatathimini kwa kufanya utafiti mblimbali ilikuwezesha mpango wa mfuko
huo kuweza kufikia malengo yake .
Alisema kuwa
takribani vijiji 9976 vimeweza kua
athiriwa natekemeko hilo ambapo watu jumla milioni 1.1 walioathiriwa na
tetemeko hilo wahitaji kiasi cha shilingi bilioni 623 ilikuwezesha mfuko huo
wamajanga kuweza kufanya kazi ipasavyo .
‘’Habari
njema kutokana makubaliano na wahisani ambapo mkataba wake ulisainiwa june
mwaka huu ni hatua nzuri za kuunganisha nguvu ilikuweza kufanya kazi vizuri ilkuweza
kutunisha mfuko huu wa majanga hii ni hatua nzuri yakuuboresha mfuko huu ‘’Aliongeza
ilomo .
KATIBU Mkuu
aliyataka mashirika yakimataifa ikiwemo benki yadunia ,DFID SIDA ,UNDP ,UNICEF
ILO pamoja UNFPA kuzidi kushirikiana
naserikali ya awamu yatano katika mipango ya maendeleo .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni