Jumanne, 4 Oktoba 2016

JAMII YATAKIWA KUZINGATIA MAZOEZI ILIKUWEZA KUKUZA UFANISI MAHALA PAKAZI .



Timothy Marko.
IMELEZWA kuwa  magonjwa mengi yasiyo ambukiza yanatokana na kuwepo kwa tabia hatarishi ikiwemo kulavyakula visivyozingata virutubisho sahihi nakwakati sahihi .

Hayo yamebainishwa leo na Mkurugenzi wa Taasisi ya impact afya Dk.Fred Mushiri wakati akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es salaam ambapo amesema magonjwa mengi yasiyo ambukiza yatokana na mtindo wa maisha ikiwemo kula vyakula hivyo pasipo kufanya mazoezi .

‘’Suala zima la lishe na kutofanya mazoezi sio kitu kizuri kwani nihatari kwa afya hali inayochangia ongezeko lauzito ,lishe bora ni ile kiasi gani na kwawakati gani ‘’Alisema Dk.Fred Mushiri .

Dk Mushiri alisema kuwa kutokana na kuwepo kwa ongezeko la watu wanaokabiliwa namagonjwa yasiyo ambukiza kwa kiasi kikubwa taasisi yake ya impact afya imeanza kutoa elimu kwa taasisi mbalimbali kuweza kutenga muda kwa wafanyakazi wao muda wa kufanya mazoezi.

Alisema ilikuweza kukabiliana natatizo lamagonjwa yasiyo ambukiza jamii lazima itenge muda wamazoezi ilikuweza kuondokana namsongo wa mawazo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni