MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR ES SALAAM |
Timothy Marko
WAKAZI wa mtaa wa
Kipera Kata ya Kitunda Ilala jijini Dar es Salaam,wamelalamikia
kitendo cha ku tishiwa maisha yao na Mwenyekiti wa
Mtaa huo Hussein Yusufu (CCM).
Wakizungumza na Chanzo chetu , kwa nyakati tofauti juzi kwa masharti ya
kutokutajwa majina yao gazetini ,wakazi hao walidai kuwa
kumekuwa na vitendo vya unyanyasaji
katika mtaa huo ambavyo wamedai kuwa vinafanywa na sungusungu
kwa shinikizo la Mwenyekiti.
Walisema Sungusungu
wa mtaa huo wamekua na tabia ya kuwakamata
wananchi holela usiku pindi wanapochelewa kurudi kwenye
majukumu yao ya kazi na kuwafungia katika ofisi ya serikali
ya mtaa huku wakiwapa vipigo bila sababu.
Walisema baada kuona hali
hiyo inazidi kushamiri waliamu kumueleza
Mwenyekiti huyo ili aitishe mkutano waeleze kero zao lakini
Mwenyekiti huyo alidai kuwa hana muda.
Walisema baada ya kumtaka
Mwenyekiti huyo kuitisha mkutano wa hadhara ili waseme
kero zao, , Mwenyekiti huyo aliwajibu kwamba kazi
anayoifanya ni ya kujitolea hivyo hana nafasi ya
kufanya mkutano na wananchi na kamba waimfuatefute kuna watu
ameshawapoteza hivyo wanaoleta jeuri na kumsumbuasumbua nao atawapoteza.
“ Tunazidi kuishi kwa mashaka
kutokana na kauli za Mwenyekiti , tuna nyanyaswa katika
mtaa wetu utafikiri sisi ni wakimbizi ,tunamuomba Mkuu wa Wilaya ya
Ilala, Sophia Mjema, na OCD wa Ukonga wafike katika mtaa huu
tuwaeleze kilio chetu kwani tumechoka kunyanyaswa hatuna
amani tumekuwa kama wakimbizi,”alisema mmoja wa wananchi hao.
Waliongeza kuwa bado katika maeneo
yao wanayoishi wanaibiwa mali zao usiku pamoja na
kuchangishwa kila mwezi Sh. 2000 kwa ajili ya ulinzi
shirikishi na kwamba wanapompelekea malalamiko Mwenyekiti huyo kuhusu kuibiwa
anawajibu kwamba yeye analinda raia halindi mali.
Katika hatua nyingine wananchi
hao walisema hawana imani na Mwenyekiti huyo kwa sababu amekuwa hasikilizi kero
za wananchi wala hana muda wakuitisha mikutano.
Mmoja wa wananchi hao ambaye
alidai kuwa alikuwa mmoja wa sungusungu hao ambaye naye
hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alisema kazi hiyo ni ngumu ameamua
kuacha kwa madai kuwa pesa zinazochangishwa kwa wananchi ili walipwe wao
ni ndogo hazilingani na kazi wanayoifanya usiku .
chanzo hicho, kilimtafuta
kwa njia ya simu Mwenyekiti huyo ,ambapo aliijibu kwamba
anasikitishwa kusikia tuhuma hizo na kwamba katika uongozi
kunakuwepo na maadui wengi , hivyo anaamini wanaomtuhumu ni wale ambao
wanapiga vita uongozi wake.
Alisema sungusungu wapo katika mtaa
huo kwa mpangilio na makubaliano na wananchi wenyewe
ambao ndio walioamua kuwepo na sungusungu baada ya mtaa huo
kuvamiwa na majambazi ndipo wananchi walikubaliana na Mwenyekiti
huyo kuwepo na ulinzi shirikishi na watoe kiasi cha fedha cha
kuwalipa walinzi hao.
“Siasa naijua waliokupa taarifa
hizo wanataka ushindi kuiharibu serikali yangu, wananisingizia kwamba
siitishi mikutano ndgu mwandishi mimi kila baada ya siku kadhaa naitisha
mikutano au vikao, pia madai ya mimi kutoa kauli ya kupoteza
mtu kama wanavyodai , sijawahi kupoteza mtu ila kama ni kijana
wangu hata kama nimemzaa akifanya uhalifu siwezi kumtetea,”alisema Yusufu
nakuongeza;
“Nasikitika sana kuona sehemu yenye
utendaji mzuri ikipakwa matope ,mimi si tetereki siasa naijua, sungusungu
wanafanya kazi kwa matakwa ya
wananchi atakaye kamatwa usiku wa manane halafu akawa mkorofi
kwa walinzi lazima atawekwa
sehemu mpaka asubuhi ntajua
nichukue maamuzi ya kumkanya
au kumchukulia hatua za kisheria,”alisema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni