kamishina wa kanda maalum CP SIMON SIRRO. |
Timothy
Marko .
JESHI
lapolisi kanda Maalumu jijini Dar es
salaam, limewataka wananchi kutumia namba za utoaji taarifa kwajeshi hilo kwa
uangalifu mkubwa nakutoa kauli chafu zakuzalilisha jeshi hilo, pindi wanapotaka
kupata huduma za ulinzi nausalama wa raia ikiwemo kutoa taarifa za kihalifu.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Kamishina wa Kanda Maalum CP Simon
Sirro amesema kuwa kumekuwa namatumizi mabaya yanamba zinazotolewa na jeshi
hilo ikiwemo 112 na 111 ambapo jeshi hilo limebaini kuwa baadhi ya wananchi
huzitumia namba hizo kwatutoa taarifa za uongo juu yajeshi hilo .
‘’Kumekuwa
namatumizi mabaya yanamba zetu 112 na 111 juu yakutoa taarifa za uhalifu katika
eneo husika ,Baadhi ya wananchi wamekuwa wakitoa taarifa za uongo na kutoa
lugha za matusi juu ya jeshi la polisi ninawaomba wananchi waache tabia hiyo ‘’Alisema
Kamishina Simon Sirro .
Kamishina
Sirro amesema kuwa endapo jeshi hilo litabaini kuwepo kwavitendo vidanganyifu
au vya matusi vinavyo fanywa na baadhi ya wananchi juu yajeshi hilo ,jeshi
lapolisi litwachukulia hatua watu hao na kuwapeleka katika vyombo vya sheria .
Katika hatua
nyingine Jeshi hilo limewataka Wenyeviti waserikali za mitaa kuwa makini pindi
wanapowachagua vijana ama kundi linalojihusisha naulinzi shirikishi kwani
baadhi yao wamekuwa wakidaiwa kufanya vitendo vya kihalifu .
‘’Kuna
baadhi yavikundi vyaulinzi shirikishi katika maeneo ya Gongo lamboto ,vikundi
hivi shirikishi vimekuwa vikihamahama nakwenda mbagala nakufanya vitendo vya
kihalifu ,vikundi hivi nasema sio vikundi vya ulinzi shirikishi bali nivikundi
vya kihalifu ‘’.Aliongeza Sirro.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni