Jumatano, 14 Septemba 2016

JESHI LA POLISI KUWATOZA WATAKAOKIUKA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

Kamishina wa kikosi cha usalma barabarani Mohamed Mpinga
Timothy  Marko
Katika kuhakikisha suala la elimu ya usalama barabarani inazingatiwa  jeshi la polisi nchini kikosi cha usalama barabarani kinatarajia kufanya maadhimisho ya wiki nenda kwa usalama barabarani nchini, itakayofanyika mwezi October mosi huko mkoani Geita.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, kamishuna msaidizi wa kikosi cha usalma barabarani DCP Mohamed Mpinga amesema kuwa maadhimisho hayo yataenda sambamba na kauli mbiu ya HATUTAKI AJAL, TUNATAKA KUISHI SALAMA, (No road crushes, we want to live safely).

“Ongezeko la vyombo vya moto nchini kwa upande mmoja na ule wa ongezeko la watumiaji wa barabara wa ngazi mbalimbali hauna budi kutiliwa maanani, ili kuweza kuzuia ajali za barabarani” Alisema kamishina Mpinga.

Pia alisema, ajali nyingi barabarani zimekuwa zikichangiwa na wadau mbalimbali wa usalama barabarani kutojua sheria pamoja nakutumia vyombo vya moto ambavyo ni vibovu, hivyo kuathiri hali ya usalama barabarani.

Pia kauli mbiu ya mwaka huu inasisitiza kila mtuaji wa barabara kufaham wajibu wake katika kuhakikisha usalama barabarani unazingatiwa, na anasisitiza kuwa suala la usalama barabarani siyo kazi ya kundi moja tu, bali ni la kila mtu anapaswa kujiona ni muhusika.

“Wanahabari ni miongoni mwa wahusika wa suala la usalama barabarani kwani kupitia wao wana nafasi kubwa kuielemisha jamii na umma kwa ujumla ili kusaidia jitihada mbalimbali katika kujenga utamaduni wa kuheshimu sheria za uslama barabarani nchini”

Kamishina Mpinga aliongeza kuwa, wakati wa zoezi hilo jeshi la polisi kupitia kitengo cha uslama barabarani litatoa elimu kwa wadau mbalimbali wa barabara pamoja na kufanya ukaguzi wa vyombo vya moto ikiwemo magari, bajaj na pikipiki. Vilevile zoezi hili litaendana na utoaji wa stika za usalama barabarani kwa vyombo vitakavyothibitika kuwa na ubora wa kutembea barabarani.

Ambapo alivitaja viwango vya ukaguzi wa magari na kuwekea stika itakuwa katika mifumo mitatu; magari ya biashara yatatozwa shs 5000/-, wakati magari madogo ya binafsi shs 3000/-, pikipiki na bajaj shs 1000/-

Hivyo anawataka wananchi kupeleka vyombo vyao vya moto katika vituo vya polisi kikosi cha usalama barabarani kitengo cha ukaguzi wa magari ili kuweza kukaguliwa na kuhakikiwa.

“Endapo katika ukaguzi wa chombo chochote kitabainika kuwa ni kibovu, basi mmiliki anapaswa kukipeleka kwa ajili ya matengenezo, na kisha kukaguliwa kwa mara ya pili na kubandikwa stika maalum”

Wakati huo huo kampuni ya mafuta ya Puma Enegy ambayo imekuwa ikiwekeza kwa muda mrefu upande wa barabara, ambacho inaamini ni kipengere muhimu katika maendeleo ya Taifa, vilevile usalama barabarani umeendelea kuwa changamaoto kubwa  duniani hivi sasa.


Philippe Corsaletti ambaye ni Mkurugenzi mkuu wa Puma Enegy nchini amesema “tukumbuke kwamba kuwekeza katika usalama ni kujenga nguvu ya baaadaye katika nyanja zote za uwekezaji imara na kujenga uchumi endelevu kwa watu wetu”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni