Alhamisi, 11 Agosti 2016

WAZIRI NAPE ALIFUTA GAZETI LA MSETO KWA KUANDIKA HABARI ZA UCHOCHEZI.

waziri wahabari sanaa nautamaduni michezo Nape NAUYE

Timothy Marko.
SIKU chache baada yaNaibu Waziri wa ujenzi Mawasiliano na uchukuzi Mhandisi Edwine Ngonyani kulitaka Gazeti la Mseto kulipa faini yashilingi bilioni moja baada ya gazeti hilo kumhusisha na upokeaji wafedha za kufanyia kampeni katika jimbolake la Namtumbo kinyume nansheria waziri wa habari nape nauye ameamua kulifungia miaka mitatu sawa namiezi 36.

hatua hiyo ya waziri wahabari Nape kulifungia gazeti hilo imefuatia tangazo la serikali serikali 242 lililotolewa agosti 10 mwaka huu baada yakuonekana  kukiuka sheria yamagazeti mwaka 1976 sura 229  kifungu 25(1).

Aidha,uamuzi huo wa serikali umelizuia gazeti hilo kuchapwa kwanjia nyingine ikiwemo mitandaoni kufuatia sheria yakieletroniki na posta sura 306 ,waziri nape amesema kuwa hatua hiyo imechukuliwa baada msajili wa magazeti kulionya gazeti hilo tangu september 2012 hadi agost 2016 kuacha kuandika habari za uchochezi na za uongo nazisizo zingatia maadili ya uandishi wa habari.

''kutokana na hali hiyo serikali  kwamasikitiko makubwa imelazimika kuchuakua uamuzi huu kutokana namwenendo wa uandishi wagazeti hilo kuandika nakuchapisha habari yakugushi kwakutumia nyaraka mbalimbali za serikali kwania yakumchafua Rais Dk.Jonh Pombe MAGUFULI naviongozi waserikali ''Alisema WAZIRI nape nauye .

Waziri Nape alisema kuwa hivi karibuni gazeti hilo lilimchafua kiongozi huyo wanchi kwakumhusisha natuhuma za rushwa  ,hatahiyo katika uchunguzi  wake serikali ilibaini kumekuwa namtindo wakugushi nyarakazilizotumiwa kuandika habari hiyo .

''ninatoa wito kwamiliki wahari ri kuzingatia sheria  kanuni namaadili yataluma ya habari tukizingatia hayo hatutakuwa namigogoro yoyote ''Aliongeza waziri NAPE NAUYE.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni