Jumanne, 2 Agosti 2016

WATANZANIA WASHAURIWA KUWEKEZA KATIKA MASOKO YA MITAJI KUKUZA UCHUMI .

Tokeo la picha la moremi marwa

Mkurugenzi Wa Soko la Hisa la Dar es salaam MOREMI MARWA

Timothy  Marko.

WATANZANIA wameshauriwa kuwekeza katika masoko ya hisa kwa kununua hisa za makampuni mbalimbali nchini ,ilikuweza kuchangia kukukua kwa sekta yaviwanda na kuwezakukuza uchumi unaotokana na sekta hiyo.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi mtendaji wa Soko la hisa la Dar es salaam (DSE) Moremi Marwa wakati akitoa tunzo kwa kwanafunzi wa vyuo vikuu vilivyo shiliki katika shindano la schollar investment challange ambapo chuo cha uhasibu cha jijini arusha kimeibuka kuwa mshindi ,Moremi amesema kuwa kutokana nashindano hilo uelewa wa wananchi hususa masoko yamitaji nchini umekuwa mkubwa ikilinganisha na awali .
''WATANZANIA nilazima kujikita katika kuwekeza katika sekta ya viwanda kwa kukuza mitaji yao kupitia ununuzi wa hisa za makapuni ilikuweza kumiliki uchumi  kupitia sekta ya viwanda ambapo sekta hii imekuwa ikikuwa kwa kasi na kuwa kichocheo cha uchumi ''Alisema Moremi Marwa .

Mkurugenzi wa soko lahisa la Dar es salaam Moremi amesema kuwa katika utafiti ulofanywa nasoko hilo kumekuwa naongezeko kubwa kwa baadhi yawanafunzi wa vyuo vikuu  wanaonunua hisa katika soko hilo nakukuza mitaji yao ambapo takbani wanafunzi3250 waliweza kujiunga na soko hilo ikilinganishwa wanafunzi 3200 katika kipindi chamwaka jana ,hali iliyochangiwa nauelewa wamasoko ya mitaji katika kukuza uchumi .

Alisema kuwa Shindano la Schollar investment challange lililo anzishwa na  taasisi hiyo ya kifedha imeweza kukuza uelewa wanwanafunzi wa vyuo vikuu nchini nakukuza mitaji yao na kuondokana na umasikini .
''kwakutumia shindano hili la schollar investment chalange kwakuwashirikisha vyuo vikuu nchini tumeweza kukuza mijadala mbalimbali nakukuza ushiriki ambapo wanafunzi wavyuo vikuu nchini wameweza kushiriki katika mashindano mbalimbali ikiwemo Scholar investment challange ''Aliongeza Moremi Marwa.

Meneja uwekezaji katika  benki ya CRDB Francisis Marwa amesema kuwa kampuni yake imeweza kuaminiwa katika uwekezaji kupitia masoko yamitaji na hisa ambazo zinazo uzwa kutoka kwenye benki hiyo kupitia soko la hisa .
Alisema kuwa ushirikishwaji wa watanzania katika kununua hisa utaweza kukuza uchumi nakuwongezea kipato wananchi na kuondokana nahali ya  umasikini wakipato .
''SISI Kama CRDBtutaendelea kusapoti wawekezaji wandani nakuweza kusapoti katika sekta  mbalimbali ikiwemo elimu na hasa suala  la madawati ilikuhakikisha sekta yaelimu inapewa kipaumbele kama mheshimiwa Rais anavyotuagiza katika uchangiaji wamadawati ilikukuza sekta yaelimu nchini ''alisema Francis Marwa .

Mkurugenzi wa uwekezaji kupitia mifuko ya uwekezaji Sostenes Gewe amesema kuwa watanzania nilazima kutumia fursa yaununuzi wahisa kama njia yakukuza mitaji ilikuweza kukuza kipato .
Alisema nilazima Watanzania kutumia muda wao mwingi katika kuwekeza katika kununua hisa mbalimbali za makampuni ilikuweza kujiletea mafanikio yakiuchumi .
''Nilazima watanzania kujiwekekea nindhamu ya matumizi ikwemo kuweka nidhamu yamatumizi namipango ilikuweza kujiletea maendeleo yakiuchumi  ''alisema GEWE.
KATIKA hatuanyingine Mshindi wa shindano la Schollar investment katika chuocha uhasibu Mjini Arusha Godfrey Makweka amesema kuwa amekua na tabia yakuwekeza katika makapuni na ya cement kwani kumekuwa na faida kubwa katika makapuni hayo .

Alisema baada yakuwa mshindi washindano hilo anatarajia kuwa balozi wa taasisi ya DSE ilikwawezsha wadau wengine ikiwemo wanafunzi wavyuo vikuu kutumia fusa ya uwekezaji.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni