Ijumaa, 5 Agosti 2016

MAKAMBA :TANZANIA TUNA ADUI MWINGINE NAYE SIO MWINGINE NI PENGO WALIOKUWANANCHO NAWASIOKUWA NACHO.

Tokeo la picha la january makamba
Waziri wa Mazingira ofisi ya makamu wa Rais January Makamba


Timothy Marko.
KATIKA kuhakikisha jamii ya Tanzania inakuwa na usawa katika ukuwaji wauchumi, jamii imeshauriwa kuwekeza katika elimu ilikuweza kuondokana na pengo la walionacho nawasiokuwanacho ili kukuza uchumi na kukuza kipato chao 
.
Akizungumza Katika uzinduzi wa ripoti yahali ya afrika mashariki 2016 kukosekana kwa usawa katika masuala yakuiuchumi nakisiasa (The state of East Africa 2016 consolidating Misery, the political economy of inequalities) Waziri wa Mazingira ofisi ya makamu wa Rais January Makamba amesema kuwa hali ya umasikini imezidi kuwa kubwa hali inayochangiwa na hali ya kuwepo kwa pengo walionacho nawasikiuwa nacho kuwa kubwa .

‘’Changamoto kubwa tangu tupate uhuru ni umasikini,ujinga maradhi  lakini ameongezeka adui mwingine kati ya walionacho na wasikuwa nacho lakini kutkana nauzinduzi wa ripoti hii itakuwa mwarobaini wa hali ya pengo la walionacho nawasikuwa nacho ‘’Alisema Waziri wa Mazingira ofisi ya Makamu wa Rais January Makamba.

Waziri Makamba alisema kuwa hali ya kuwepo kwa pengo la walionacho nawasikuwa nacho kuongezeka limetokana na kukosekana kwa usawa wa ugawaji wa rasmali hali hiyo inapotekea nilazima viongozi wawemakini katika kudhibiti hali hiyo .

Alisema kuwa Hapo awali usawa wakipato ulikuwa unachangiwa nadhana malimbali ikiwemo Rangi ambapo jamii ya kiasia nawazungu walikuwa wakimiliki kiwango kikubwa cha Rasmali ikilinganishwa na waafrika ambao walikuwa wakimiliki kiwango kidogo cha Rasmali .

‘’KATIKA safari yanchi yetu tumepata wazungu wapya,kuna watumishi wanaishi maisha mazuri tofauti ya kipatohatuna budi kukabiliana natatizo la usawa kwa kuwekeza kwenye elimu kwani ninyenzo muhimu lakukabiliana natatizo lakukosekana kwa usawa ‘’Aliongeza WAZIRI Makamba .

Makamba aliongeza kuwa takwimu zinaonesha kuwa uchumi watanzania unakuwa siku hadi siku nilazima kuwekeza kwa elimu kwa watoto wetu ilikuondokana napengo lawalionacho nawasikuwa nacho hali itakayo chochea ukuwaji wa kiuchumi na kuondokana umasikini wakipato .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni