![]() |
MKURUGENZI WA OFISI YATAKWIMU Dk.Albina Chuwa . |
TimothMarko.
MKURUGENZI wa
ofisi ya Takwimu nchini Dk.Albina Chuwa amesema kuwa hali yautumikishwaji wa
watoto imekuwa tatizo kubwa duniani ambapo zaidi ya watoto milioni264 duniani
kote wamekuwa wakitumikishwa .
Akizungumza
katika uzinduzi wa Ripoti ya hali ya utumikishwaji wa watoto ya mwaka huu
(Child Labour )mapema hii leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi huyo amesema kuwa
watoto waliopo kati yaumri wa miaka 5-17 wamekuwa wakitumikishwa.
‘’Utafiti
unaonesha kuwa katika kipindi cha mwaka 2014/15watoto milioni 15wenye umri kati
yamiaka mitano hadi kumi nasaba ,ambapo watoto milioni 4.2 sawa na asilimia
28.8 wanatumikishwa katika kazi mbalimbali za kiuchumi.’’Alisema Mkurugenzi wa
ofisi Takwimu Dk.Albina chuwa .
Mkurugenzi
wa ofisi ya Takwimu Dk.Chuwa alisema kuwa katika Sekta ya kilimo ,Misitu na
uvuvi imeendelea kuwa sekta inayo ajiri watoto wengi zaidi kwakiwango cha
asilimia 92.1 ya watoto wote wanaojihusisha nashughuli za kiuchumi .
Alisema kuwa
Watoto wengi hutumia zaidi ya nusu yamuda wao katika siku katika shughuli za
kujihudumia zaidi ikiwemo kujihudumia nausafi huku wasichana wakitumia muda huo
katika shughuli za usafi nahuduma zinginezo .
‘’Asilimia
58.8 ya watoto wakiwemo wasichana hutumia muda muda mwingi zaidi katika usafi
nashughuli binafsi ikilinganishwa na wavulana ambapo hutumia asilimia 58.3
katika shughuli za kujisomea ‘’.Aliongeza Dk.CHUWA .
Naibu Waziri
Ofisi ya waziri Mkuu Sera,Bunge ,Kazi ,Vijana ,ajira nawatu wenye ulemavuDk.Abdallah
Possy amesema kuwa serikali itaendelea
kupambana vikali nakupinga utumikishaji wa watoto kwa kuanzisha progaramu ya
elimu bure ilikuweza kuhamasisha mahudhurio shuleni .
Alisema kuwa
ili kuweza kupunguza ajira za utotoni serikali inawataka kwa wazazi na walezi
kutumia vyema fursa katika kuwapeleka watoto shule ilikuondokana natatizo
lamimba mashuleni ,na ajira za watoto .
‘’niwaombe Shirika
la kazi Duniani ILO Kuendelea kushirikiana na ofisi ya takwimu ilikufanya
uchambuzi zaidi wakitalamu ilikupata makadirio yaviwango vya utumikishawaji wa
watoto katika ngazi za chini ‘’Aliongeza Dk.Possy.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni