Rais Paul Kagame Wa RWANDA |
Timothy
Marko.
RAIS wa Nchi
ya Rwanda Paul Kagame , anatarajiwa kuzindua Maonesho ya wafanyabishara ya
kimataifa ya saba saba yaliyopo katika viwanja vya mwalimu nyerere jijini Dar
es salaam.
Akizungumza na Waandishi wa habari mapema jijini
Dar es salaam Waziri wa Mambo yanje na utengamano wa kikanda wa jumuhia ya
Afrika Mashariki Balozi Agustino Mahiga
amesema Rais huyo wa Rwanda anatarajiwa kuwawasili julai mosi mwaka huu ambapo
ananatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonesho hayo ya kibiashara nchini .
‘’Ujio wa
Rais huyu wakutoka nchini Rwanda umekuja baada ya Rais wa awamu ya Tano wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jonh Magufuli Kumuomba Rais Paul Kagame wa
RWANDA kuja kutembelea nchi ya Tanzania ilikuweza kudumisha ushirikiano wa
kikanda wa wan chi hizi mbili katika jumuhia ya Afrika Mashariki ‘’Alisema Balozi Agustino Mahiga .
Waziri
Mahiga alisema kuwa sambamba na ujio huo wa Rais huyo wa Rwanda hapa nchini
,serikali imeweza kupata msaada wa madawati takribani 300 kutoka katika nchi ya
Kuweit ikiwa juhudi za serikali katika kupambana na tatizo la madawati nchini .
Alisema Msaada
huo umekuja baada ya Rais Magufuli kuzitaka balozi za nje ya nchi kuweza kukutatana nawadau
mbalimbali ilikuweza kuinua kiwango chaelimu ikiwemo kuangalia uwezekano wa
upatikanaji wa madawati ilikuondokana na tatizo la upungufu wa madawati .
‘’Kufuatia
zoezi hili za uchangiaji wa madawati nakuzitaka taasisi za nje kuweza kuchangia
madawati ilikuondokana natatizo la wanafunzi wetu kukaa chini tumeweza kupata
maombi mbalimbali kuweza kuchangia
madawati nchini ‘’Aliongeza Balozi Mahiga.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni