Timothy
Marko.
HATIMAYE Chama
cha Mapinduzi CCM kimewasilisha taarifa za Gharama za uchaguzi ulifanyika
25october mwaka jana ambapo taarifa hizo zikijumuisha Madiwani Ubunge Pamoja na
Urais .
Akizungumza
na waandishi wa habari katika makabidhiano ya taarifa za gharama za uchaguzi
Mapema hii leo jijini Dar es salaam Mkaguzi wa ndani wa chama hicho Stanslaus
Mamilo amesema kuwa hatua hiyo inafuatia utekelezaji wa masuala ya kisheria ya
sheria yauchaguzi inayowataka vyama vya vya siasa kuwasilisha gharama za
uchaguzi mara baada ya uchaguzi kumalizika .
‘’Sisi kama
chama chamapinduzi tunazingatia matakwa ya kisheria ikiwemo Gharama za uchaguzi
ambapo taarifa hizi za gharama za uchaguzi hukokotolewa na Mkuu wa mahesabu
ndani ya chama nakuwasilisha katika tume
ya uchaguzi ‘’Alisema Mkaguzi wa Mahesabu Stanslaus Mamilo .
Mamilo
alisema kuwa Makabrasha hayo hupokewa na kitengo cha masijala yatumehiyo ikiwa
niutekelezwaji wa gharama hizo zauchaguzi .
Katika hatua
nyingine Mkuu wa masijala wa Tume ya Uchaguzi (NEC)Glacia Simbachawe amesema kuwa hadi kufikia mchana wa leo
nitakrbani vyama viwili tu ndio vilivyo wasilisha gharama za uchaguzi ambapo
chama cha mapinduzi kinaongoza kikifuatiwa na chama ACT Wazelendo
.
Msemaji wa
Tume ya uchaguzi nchini Monica Laurenti alivitaka vyama vyasiasa nchini
kuwezakuwasilisha gharama za uchaguzi katika tumehiyo
.
Alisema kuwa
vyama ambavyo vitaonekana vimevuka gharama za uchaguzi zitapelekwa kwa Mkaguzi
mkuu wa mahesabu ya serikali nakuweza kuwasilishwa kwa Mwanasheria Mkuu ili
hatua za kinidhamu zichukuliwe .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni