MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA JAJI FRANCISIS MTUNGI |
TimothyMarko.
SIKUMOJA
KUPITA kauli ya Rais Dk.Jonh Pombe Magufuli yakuwataka wanasiasa kuachana
kupiga siasa na badala yake kujikita katika shuguli za kimaendeleo ,Msajili wa
vyama vya siasa Jaji Francisis Mutungi amevitaka vyama vyasiasa pamoja na viongozi
wa vyama hivyo kutafuta tafsiri ya Rais Magufuli ili kuweza kuichambua kauli
hiyo kwakina.
Akizungumza
na waandishi wa Habari mapema jijini Dar es salam Jaji Francis Mutungi amesema kuwa kauli ya Rais Magufuli
inaelekeza kuachana nasiasa zisizo kuwa natija katika kuleta maendeleo ‘’siasa
za viini macho ‘’ nakusisitiza hata nchi zinazo fanya demokarisia zinakuwa na
kikomo cha kufanya mambo yake .
‘’Tatizo
nilalo liona hapa sio Rais Magufuli kuzuia mikutano yakisiasa tatizo nitafusiri
yakile alicho kizungumza Rais ila kwa mimi tafsiri yangu sio kama amezuia
kufanyika ila ninachokiona Rais anataka kushirikana katika kuleta maendeleo ‘’Alisema
Jaji Francis Mutungi .
Jaji Mutungi
alisema kuwa nilazima kutafakari na kuweza kuyachambua mambo kama wanasiasa
nakuweza kuleta suluhisho ni nini Rais alikuwa na anakimanisha nahatimaye
kuliletea suluhishi jambo hilo nakuachana na kukurupuka .
Alisema
Katika Dunia hii nilazima kutafakari kwa kina maneno yanayotolewa na Waandishi
wa Habari ,Wanasiasa na Wanasheria nakuyatafakari maneno yao kwa Mstakabali wa
taifa.
‘’Tumefikia
Mahali Rais anataka kila mmoja wetu tushiriki katika shughuli za maendeleo
nilazima anapo ongea Rais tuweze kuzifanyia tafiti kauli zake nakuweza
kuzitafutia majibu ya kauli zake baada ya kuzifanyia utafiti ‘’Aliongeza Jaji
Mutungi .
Jaji Mtungi
aliongeza kuwa nilazima wanasiasa wajiulize
kwakipindi hiki je siasa zina tija
katika taifa letu niniachokiona Rais Magufuli anataka tufanyekazi .
.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni