Ijumaa, 1 Aprili 2016

JESHI LA POLISI LATOA MIEZI MITATU KWA WAMILIKI WA SILAHA NCHINI.

Tokeo la picha la nsato marijani

Timothy Marko.
JESHI la polisi nchini limetoa miezi mitatu kwa wananchi wanaomiliki silaha kuhakiki silaha zao nakulipa ada ya umliki wa silaha hizo .

Akizungumza na Waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar es salaam Kamishina wa operesheni na mafunzo CP Nsato Mssanzya amesema kuwa Hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa mkanganyiko wa operesheni yaukaguzi wasilaha hizo kwa mikoa mbalimbali nchini.

‘’ZOEZI laukaguzi wasilaha  limekuwa rikiratibiwa nakila mkoa kwakutoa muda wake kibinafsi jambo ambalo limeleta mkanganyiko katika utekelezaji wa zoezi hilo kwa baadhi ya wamiliki ‘’Alisema Kamishina waoperesheni na mafunzo CP Nsato Mssanzya .

Alisema kuwa sambamba nazoezi hilo pia jeshi hilo limewatahadharisha wananchi kuwa makini navitendo vya kihalifu katika maeneo yao ikiwemo kubaini makundi mbalimbali ya kihalifu katika maeneo  yao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni