Alhamisi, 31 Machi 2016

TPDC:ZAIDI YA ASILIMIA 75 YAWATALAMU WA SEKTA YAGESI NI WAZAWA .



Timothy Marko.
SHIRIKA la Maendeleo ya petrol nchini (TPDC)limesema kuwa zaidi ya asilimia 75 ya wachimbaji wa gesi ni wazawa ambapo watanzania hao hushiriki shughuli za kitalaam ikiwemo (floormen)

Akizungumza katika mahojiano maaluum waandishi wa habari Afisa maendeleo ya jamii Osca Mwakasege amesema kuwa wazawa hao hupata utalaam wa uchimbaji wa gesi katika maeneo ya baharini .

‘’watalamu wazawa hupataujuzi hupata ujuzi kulingana naviwango vya kimataifa katika sekta yautafutaji wa gesi asilia ‘’Alisema afisa Maendeleo ya jamii Osca Mwakasege

Mwakasege alisema kuwa licha yasilimia hiyo 75 bado ushiriki wa wazawa katika ushiriki wauchimbaji wa gesi bado umeonekana kuwa ni mdogo hali inayo changiwa na ukosefu wa elimu .

Alisema kuwa kufuatia uhaba wa watalaam hao taasisi hiyo imeamua kuwasomesha watalamu wazawa ilikuweza kufidia kiwango hicho kidogo cha watalamu .

‘’lengo lakuwasomesha watalamu hawa nikuwa wawezesha watalamu wazawa waweze kuajiliwa katika sekta ndogo siku za usoni ‘’Aliongeza Mwakasege.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni