Timothy Marko.
WAZIRI wa elimu na mafunzo ya ufundi
nchini Jocyce Njalichako amemuondoa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo
George Nyatega baada ya kutotoa mikopo ya wanafunzi kwa wakati.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam waziri Njalichako amesema kuwa wanafunzi 23 waliweza
kupata mikopo katika vyuo viwili tofauti kwa kipindo cha miaka mitatu mfululizo
.
"jumla ya sh 153,999,590 ambazo
zililipwa kwa chuo cha kwanza wakati huohuo chuo cha pili kilipwa sh
147,541,460 katika ya wanafunzi 169" alisema Njalichako
WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YAUFUNDI STADI JOYCE NDALICHAKO . |
WAZIRI Njalichako alisema kuwa jumla
ya wanafunzi 343 wasiokuwa na usajiri kwenye vyuo husika waliweza kulipwa jumla
ya sh 342,468,500 wakati huohuo wanafunzi 55 walioacha masomo walilipa kumla ya
sh 136,232,800.
Alisema kuwa takribani jumla ya sh
159,664,500 zililipwa kwa wanafunzi 306 ambao ni kiwango kilichobainishwa
kwenye vipengere namba 4 .3 na 4.3.2 cha miongozo ya ukopeshaji wa mwaka
2008,2009.
" kwa mujibu wa kifungu D.5(3)
cha kanuni za kudumu kinachohusu uteuzi wa maofisa wa serikali pamoja na
kifungu D 12 kinachohusu taarifa za mtendaji na kifungu f.50(1) kinachohusu
usitishaji wa mkataba kwako mawaziri nimemsitisha mkataba wa ajira bw George
Nyatega kama mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mikopo" aliongeza
WAZIRI Ndalichako katika hatua
nyingine amewasimamisha Yusuphu Kisela ambaye no mkurugenzi wa fedha na
utawala, Juma Changoja ambaye ni Mkurugezi wa uwezeshaji mikopo pia amsitisha
Onesmo Laiza ambaye no mkurugenzi wa upangaji na utoaji mikopo wa bodies hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni