Jumatatu, 15 Februari 2016

WAFANYAKAZI WA MWALIMU NYERERE SQUIRE WAMLAMIKIA MKANDARASI WAKICHINA KUWALIPA SHILINGI 5000



Timothy Marko.
WAFANYAKAZI wa ujenzi wajengo la Mwalimu Nyerere(CRJ) SQUIRE wamemlalamikia mkandarasi wa jengo hilo kwa kutowalipa stahiki zao kwa wakati nawakati huo huo wamemlalamikia mkandarasi huyo kwakuwalipa shilingi 5000 kwasiku hali inayofanya wafanyakazi hao kutokidhi mahitaji yao 
.

HAYATI MWALIMU NYERERE

Akizungumza kwaniaba ya wafanyakazi wenzake wajengo hilo Kelvin Roman amesema kuwa kutokana na wafanya kazi hao kutopewa mikataba yao kwa kipindi cha muda mrefu kwenye ujenzi unao endelea katika jengo hilo hali ilichangiwa kutolipwa kwa wakati .

‘’Tatizo la msingi ndugu mwandishi nibaada ya taarifa ya wizara ya ajira kuwataka wajiri wote watoe mikataba kwa wafanyakazi wao ,tunachokihitaji sisi hapa nikupewa mikataba yetu  ya ajira inayozingatia vigezo vyote vya mkataba ‘’Alisema Kelvin Roman .

Kelvin alisema kuwa hivi karibuni waziri wa ujenzi profesa Makame Mbarawa alitaka katika sekta ya ujenzi wafanyakazi wote wapewe mikataba .
Alisema kuwa wamepewa mikataba ambayo haioneshi lini wafanyakazi hao walianza kazi nakusisitiza kuwa mikataba hiyo imekuwa ikitolewa kwa kificho kwa baadhi ya wafanyakazi
‘’Mikataba haioneshi lini mfanyakzi alianza kazi ,nawala mkataba huu unasema utalipwa kwawiki hali inayo changia sitofahamu na ajira zetu ‘’Alisema Kelvin Roman.
Meneja Rasmali watu wa kampuni ya CRJ anaye jenga jengo hilo Tatina Yang amesema kuwa ameweza kufuata maelekezo yaserikali lakini kinachosekana katika kampuni yake ni uelewa mdogo wa masuala ya mikataba katika makampuni .
Alisema kuwa kinachofuata sasa nikuwasikiliza matatizo yao ili tuweze kuweza kuyatatua kwa kusanya maoni yao.
‘’Kama kampuni hii itafungwa wafanyakazi watakosa ajira na watu hawa hawatakidhi mahitaji yao ‘’Alisema Yang.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni