Blogu hii makini iko kwa ajili ya kuhabarisha masuala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Karibuni sana.
Alhamisi, 26 Novemba 2015
WADAU WA SEKTA YA VIWANDA WAASWA KUTUMIA DHANA YA KAIZEN ILI KUKUZA SEKTA HIYO NCHINI.
Timothy Marko.
KATIKA kuhakikisha sekta ya viwanda inakuwa na kuleta tija kwa taifa katika uchumi Tanzania inatarajia kukutana na wadau mbalimbali katika kuadhimisha siku ya Kaizen Inayotarajiawa kuadhishwa 30 Novembar mwaka huu .
Katika maadhimisho hayo yasiku kaizen yanalenga juu yautekelezaji wa dhana mbalimbali zilizojengwa na wanafalsafa huyo wakutoka nchini japan ambapo watalamu mbalimbali wasekta hiyo ya viwanda katika kujenga uchumi kutokana na sekta ya viwanda .
Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa wizara ya viwanda na biashara Uledi Mussa amesema kuwa maadhimisho hayo yanalenga kuwakumbusha wataalamu wa sekta hiyo katika kukuza ubora wa bidhaa na kuongeza tija .
‘’Dhana ya kaizen tunatarajia kuitekeleza ambapo asili ya dhana hii nikutoka nchini Japan ,nchi hii imeweza kukua katika viwanda kwakutekeleza dhana hii nasisi Tanzania tutashirikiana na nchi ya Japan katika kutekeleza dhana hii ‘’Alisema Katibu Mkuu Uledi Mussa.
Katibu waviwanda na biashara Uledi Mussa alisema kuwa dhana hiyo ya KAIZEN inatarajiwa kutekelezwa katika mikoa mitatu ambayo ni Dar es salaam ,Morogoro ,pamoja na DODOMA .
Alisema kuwa katika utekelezaji wadhana hiyo ya KAIZEN inalenga kukuza sekta binafsi za viwanda ambapo viwanda vyandani yanchi ndio mdau muhimu wa dhana hiyo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni