Blogu hii makini iko kwa ajili ya kuhabarisha masuala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Karibuni sana.
Jumatano, 25 Novemba 2015
SERIKALI :HATUTO INGIA GHARAMA ZA POSHO ZA VIKAO .
Timothy Marko.
SERIKALI imesemakuwa haitaingia gharama juu ya uendeshaji wa vikao vya kazi kwa watumishi wake ikiwemo kukodi ukumbi ,usafiri na muda wa vikao vya nje na badalayake itatumia mfumo wa tehama katika kuendesha vikao hivyo .
Akizungumza na waandishi wa Habari mapema hii leo jijini Dar es salam ,Mkuu wakitengo cha mawasiliano serikalini ofisi ya utumishi wa umma Florence Temba amesema kuwa vikao vyote vya kazi vya wakurugenzi ,makatibu tawala wamikoa ,maaafisa utumishi wa mamlaka za serikali za mitaa.
‘’Vikaokazi vitaendeshwa kwa kutumia mfumo wa mawasiliano ya Video conference ambapo kikao kimoja kinaunganishwa kwa washiriki kutoka mikoa nane ambapo maada huwasilishwa nakutoa fursa ya kuwasiliana moja kwa moja kwa maswali au ufafanuzi ‘’Alisema Florence Temba .
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Serikalini Florence Temba alisema kuwa kupitia utaratibu huo utawawezesha washiriki kubaki katika maeneo yao yakazi na kutokuwa nagharama ya usafiri ama kukuodi ukumbi kama ilivyokuwa awali .
Alisema kuwa muda utakao tumika katika kuendesha vikao hivyo utatumia masaa matano na mwenyekiti wavikao hivyo nikatibu mkuu ,ofisi yarais Menejimenti ya utumishi wa umma .
‘’Mfumo huu nisalama kwasababu miundo mbinu yote inayotumiwa inaratidiwa na serikali ambayo ina miundombinu ya Tehama ‘’Aliongeza Florence Temba.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni