Timothy MarkoMFUMUKO wa bei katika kipindi cha mwezi Oktoba umeongezeka hadi kufikia asilimia 6.3 kutoka asilimia asilimia 6.1 ikilinganishwa nakipindi cha mwezi septemba ambapo kasi ya upandaji wa huduma za bidhaa imeweza kupanda katika kipindi cha mwezi Oktobar .
WAKATI huohuo,Farihisi za bei zimeongezeka kutoka 149.70 hadi kufikia 159.17 na mfumuko wa bei bei za bidhaa za vyakula navinjwaji baridi umewezakuongezeka kutoka asilimia 9.6 hadi 10.2 ikilinganishwa kipindi cha mwezi septembar .
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Mkurugenzi wa sensa za watu na uchumi Ephraim KUSIGABO amesema kuwa ongezeko hilo limeweza kuchangiwa naongezeko la bei zisizo za bidhaa za vyakula kwa kipindi kinacho kishia mwezi oktobar mwaka huu ilkinganishwa nakipindi cha mwaka jana.
'' Mwenendo wa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula zilizooneshwa kuongezeka katika kipindi cha mwezi Oktober mwaka huu ikilinganishwa na mwezi oktober mwaka jana nipamoja bei za mchele kwa asilimia 28.3,mihogo mibichi kwa asilimia 19.0 wakati samaki ikiwa ni asilimia 15.9''Alisema Ephraim Kusigabo.
KUSIGABO alisema kuwa ikilinganishwa namfumuko wa bei katika nchi za ukanda wa afrika mashariki kenya umeongezeka kwa asilimia 6.72 kutoka 5.97ikilinganishwa nanchi yauganda asilimia 8.8 kutoka asilimia 7.2 kwa kipindi cha septembar mwaka huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni