Timothy Marko.
CHAMA cha wananchi CUF tawi la zanzibar kimesema kuwa kimeshangazwa na hatua ya tume ya uchaguzi visiwani humo (ZEC)kutengua matokeo ya uchaguzi mkuu ulikuwa unaendelea visiwani humo baada ya kura kuhesabiwa na kuonekana chama hicho kimepata ushindi kati ya majimbo 54 yaliopo unguja na pemba.
Hatua ya kutenguliwa matokeo hayo yaliyofanywa na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Visiwani humo (ZEC) Jecha Salim Jecha chama hicho kimeukataa uamuzi wa mwenyekiti huyo kwa kutengua matokeo ya uchaguzi kuwa nikinyume cha sheria ya uchaguzi .
Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa wakilishi wa wateule kupitia chama hicho visiwani zanzibar Abubakar khamis Bakary amesema kuwa mwenyekiti huyo wa tume ya uchaguzi visiwani humo Jecha Salimu Jecha anatambuwa wazi kuwa kutokana nakifungu cha katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984 hakimpi mamlaka ya yakutengua matokeo ya uchaguzi visiwani humo.
''JECHA mwenyewe analitambua kuwa hilo ndio maana katika tamko lake alishindwa kifungu chochote cha katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 au sheria yauchaguzi ya zanzibar namb11 ya mwaka 1984 kinachompa uwezo wa kufuta uchaguzi wa wananchi wa zanzibar iwe ni kwake yeye kama mwenyekiti au hata kwa tume kwa ujumla wake''Alisema Mwenyekiti Abubakar Hamis BAKARI .
ABUBAKAR BAKARI alisema kuwa jambo lakushangazwa uchaguzi huo wa visiwani humo ulifanyika sambamba na ule wabunge wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wanaotokea katika majimbo ya Zanzibar nakusitiza kuwa uchaguzi huo ulifanywa siku moja kwa kutumia daftari moja la wapigia kura na kuhoji kuwa utawezaje kusema uchaguzi wa wabunge wa zanzibar ulikuwa halali nausio kuwa na dosari nawakati huo huo kulikuwa na madai uchaguzi wa wakilishi haukuwa halali naufutwe .
ALISEMA kuwa kutokana namkanganyiko huo Chama cha CUF visiwani Zanzibar kimeutaka tume hiyo yauchaguzi kutengua tamko lililo tolewa na na mwenyekiti watume hiyo ilikuweza kurahhisisha mchakato wa jumlishwaji wa kura za urais visiwani humo nakuweza kutibitishwa na baraza lawakilishi visiwani humo kwamujibu wa katiba ya zanzibar.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni