Blogu hii makini iko kwa ajili ya kuhabarisha masuala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Karibuni sana.
Jumanne, 17 Novemba 2015
SERIKALI KUENDESHA BOMOABOMOA MAENEO YASIO RASMI
Timothy Marko .
SERIKALI imesema kuwa itashirikiana na Manispaa ya kinondoni katika kuendesha operesheni maalum ya ubomoaji wa nyumba zilizojengwa kinyume na taratibu za ujenzi .
Akizunguza na waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar es salaam Kamishina Msaidizi wa ardhi Mathew Nhonge amesema kuwa ubomoaji huo unafuatiwa baada ya tamko la sera ya ardhi ya mwaka 1995 inayowataka watumiaji wa ardhi kuheshimu maeneo maalumu yaliyotengwa yasiweze kuvamiwa .
‘’Kufuatia tamko lasera namba sita yataifa ya ardhi ya mwaka 1995 ,pamoja na tamko lasera namba nane linaanisha wazi kuwa serikali za mitaa itashirikiana wizara ya ardhi ilkuweza kuhakikisha usimamizi mazubuti wa ardhi ‘’Alisema Kamishina Msadizi wa ardhi Mathew Nhonge .
Kamishina Nhonge alisema kuwa kufuatia matamko yasera hizo za ardhi kuanishwa serikali itashirikiana na manispaa ya kinondoni kuendesha zoezi la ubomoaji .
Alisema kuwa zoezi hilo litajumuisha nyumba zote ambazo zimejengwa bila kufuata kibali cha ujenzi ,michoro yamipangomiji pamoja na kutozingatiwa matumizi sahihi ya ardhi .
‘’Zoezi hili laubomoaji litajumuisha maeneo yafuatayo mbezi ,Tegeta ,Bunju,Mwenge ,BIAFRA ,kinondoni, zoezi hili linarajiwa kuanza18 jumatano ya mwezi huu ‘’aliongeza Nhonge.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni