Jumatatu, 31 Agosti 2015

BENKI YA CRDB YAONGOZA KWA UNUNUZI WA HISA JIJINI DAR ES SALAAM.

Timothy Marko.Kiwango cha ununuzi wa soko la hisa jijini kimepanda kutoka shilingi bilioni 17hadi shilingi bilioni 29 kwakipindi cha wiki iliyopita.
Akizungumza mapema hii leo jijini Dar es salalam,Meneja biashara na Masoko wa soko lahisa la Dar es salaam (DSE) Patrick Mususa amesema kuwa kiwango hicho kimeongezeka kutokana na kuongezeka kwa hisa za makapuni CRDB,TBL,TLB,wakati makapuni mengine nipamoja na USL,NMB,swisport .
''Makampuni yaliyoongoza nipamoja na CRDB ikiwa na hisa 73,TBL14,TLG 10, ambapo makampuni mengine ni pamoja na USL,NMB, naswisport ''Alisema Partick Mususa.
Mususa alisema kuwa kutokana kupanda kwa idadi ya mauzo yahisa kwa asilimia 17 ambapo jumla shilingi bilioni 22.5 zimeongezeka ikilinganishwa shilingi biloni 21.8 kwa kipindi chawiki iliyopita.
Alisema Hali hiyo imechangiwa na baadhi ya wanunuzi wa hisa kutumia huduma za mawasiliano kwa njia ya simu ambapo mteja anaweza kutumia simu ya mkononi kwa kubonyeza *150*36\\ ilikuweza kupata huduma hiyo. .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni