Timothy Marko
JESHI la
polisi kanda maalum jijini Dar es salaam
linamshikilia SIMON MEENA (40)mkazi wa Kinyerezi Segerea kwatuhuma za kuwasumbua
wafanyabiashara mbalimbali mjini hapa
kwa kuwa kuwasingizia pamoja nakuwatuhumu kwamba wanahusika na makosa yenye kuhatarisha usalama .
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini mapema hii leo Kamishina wa polisi kanda maalum
jijini Dar es salaam Suleiman Kova amesema kuwa kwakipindi kirefu jeshi lake
limekuwa likimtafuta mtu huyo baada ya kupata malalamiko mengi kutoka kwa
wananchi nauchunguzi unaonesha kuwa jina lamtu huyo halipo kwenye orodha
yawatumishi wa idara ya usalama wataifa .
‘’Tukio la
mwisho lililomfanya akamatwe ni pale alipomtishia mfanyabishara mwenye asili
yakisomali ABDI Mohamed Dalmar katika
tishio hilo la kutishia mtuhumiwa GUNNER SIMON Meena Ambaye ni afisa usalama ‘’feki’’
Alidaiwa kiasi chafedha za kitanzania
TSHS 25000,000 amasivyo ange chukuliwa hatua chini ya sheria ya usalama wa
taifa ‘’Alisema Suileman Kova .
Kamanda kova
alisema baada ya mlalamikaji kutoa taarifa katika jeshi lapolisi ndipo jeshi
hilo likaweka mtego ilkuweza kufanya uchunguzi zaidi wa shauri hilo ilkuweza kufikisha mtuhumiwa huyo mahakamani
na badaye jalada lake kufikishwa kwa mwanasheria wa serikali .
Katika hatua
nyingine Jeshi lapolisi kanda maalum jijini Dar es salaam linawashikilia watu
tisa kwatuhuma za ujambazi wakiwa na bastola moja aina ya BROWNING ambapo namba
zake zikiwa zimefutwa ikiwa na risasi 11 ndani ya magazine huko segerea majira
ya saa nane usiku septemba 2 mwaka huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni