Alhamisi, 14 Agosti 2014

RAIS KIKWETE AWATAKA WATANZANIA WAISHIO NJE YA NCHI KUWEKEZA KIUCHUMI KATIKA NCHI YAO.


Timothy Marko.
RAIS Jakaya kikwete amewataka watanzania wa naoishi nchi za nje kuwekeza  katika nchi yao ilikujieletea maendeleo kama wanavyo fanya raia wanchi za kigeni wa napotembelea katika nchi ya Tanzania nakusititza kuwa hata mataifa mengine yamekuwa  kiuchumi kwa sababu ya uwekeza ji wa rasmali zao katika nchi zao.
Akizungumza katika mkutano wa watanzania wanaoishi nje yanchi mapema hii leo katika jiji la Dar es salaam Rais Kikwete amesema kuwa ni vema watanzania hao wa ishio nje yanchi kuikumbuka nchi ya o kwani nyumbani nyumbani nakusistiza kuwa inakaririwa zaidi yadola milioni 10.2 huja kuwekeza hapa nchini  ikilinganishwa na nchi yakenya ambapo raia wanaoishi ughaibuni huchangia pato lataifa zaidi ya dola bilioni 1.3
‘’Sisi hatutakuwa wakwanza kufanya hivyo nchi nyingi duniani zimekuw a zikifanya hivyo wenzetu wanafanya hivyo nawamekuwa wakinufaika nchi nyingi zimekuwazikifanya hivyo nakuweza kukuza pato lao la ndani na kukuza uchumi ‘’Alisema Rais kikwete.
Rais kikwete alisema inakaririwa zaidi ya watu milioni 200 wanaishi nchi ambazo si za kwao nakumekuwa na idadi ndogo ya watanzania wanao ishi nchi za nje hii nikutokana nahali yakisiasa kuwa nzuri ikilinganishwa na nchi zingine nakusistiza kuwa idadi kubwa ya watanzania wanao kwenda nje nikwaminadi ya kiuchumi na kielimu ikilinganishwa na wananchi wanchi zingine wengi hukuimbilia nchiza ugaibuni kutokana na machafuko ya nchi zao .
Alisema hivi karibuni alitoa maagizo katika wizara ya nyumba na makazi ili watu waishio nchi za nje (diaspora )kuweza kupatiwa aridhi kwa jili ya kujenga nyumba nakusisitiza kuwa swala lauraia wanchimbili ambao umekuwa ukizungumziwa nchinyingi zimekuwa zinafanya suala hilo lakini suala hilo halikujitokeza kwenye rasmu ya kwanza yakatiba mpya .
‘’watanzania suala hili la uraia wanchi mbili halija wakere keta kama mambo mengine kwenye mchakato wa katiba lakini nyinyi nawaomba mjitahidi kulisemea suala hili lakini sauti yenu haisiki sana ‘’Aliongeza Rais kikwete .
Katika hatua nyingine Rais KIKWETE alisema watanzania walioko ndani na nje yanchi wanawajibu wakuchangia maendeleo yanchi yao ikiwemo kuleta mitaji ,teknolojia,maarifa,ufumbuzi wa zana na vifaa nakusistiza kuwa masoko yabidhaa nimuhimu katika kujiletea maendeleo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni