Timothy Marko.
KUFUATIA
kuwepo kwa tuhuma za kuwepo kwa vyuo vingi vinavyotoka nje ya ya Tanzania
kutokuwa na ubora unaotakiwa kwa hapa nchini chuo kikuu cha kampala cha nchini Uganda
tawi la Dar es salaam KAMPALA INTERNATIONAL UNIVERSITY (KIU)kimekanusha madai
hayo na kueleza kuwa chuo hicho kimepata ithibati nakusajiliwa kutoka tume ya
vyuo vikuu hapa nchini (TCU).
Akizungumza na
waandishi wa wahabari jijini leo,Mkurugenzi wa masoko na mahusiano ya umma wa
chuo hicho cha KIU ,Thomas some amesema
kuwa tuhuma zinazotollewa na baadhi ya watu kuhusiana na usajili wa chuo hicho
si za kweli nakubainisha kuwa kumekuwa na baadhi ya wafanyakazi walio fukuzwa
chuoni hapo wamekuwa wakichafua taswira ya chuo hicho .
‘’kumekuwa
na baadhi ya wafanyakazi walifukuzwa kazi kwa utovu wa nidhamu wamekuwa
wakieneza tuhuma juu ya chuo chetu lakini tuhuma hizi siza kweli kwani chuo
chetu kinatambuliwa na tume ya vyuo vikuu Tanzania commission university (TCU)’’alisema
Thomas some .
Thomas Some
alieleza kuwa hivi karibuni kumekuwa na baadhi ya wahitimu waliomaliza chuoni
hapo nakuweza kuajiliwa katika hospitali ya taifa yamuhimbili kwa ngazi ya
uangalizi wa madawa medical .
Some
alisisitiza kuwa hivi karibuni Raisi mstaafu wa awamu ya pili ALLY Hassan
Mwinyi alikubali kwa dhamira yake kuwa mshauri wambo ya kitaluma chuoni hapo
nakusisitiza kuwa kama chuo hicho kisinge kuwa na ithibati Rais huyo wa awamu yapili
hapa nchini asingeweza kukubali kuwa mshauri wa chuo hicho ili hali chuo hicho
hakitambuliki na tume ya vyuo vikuu TCU hapa nchini.
‘’HIVI
karibuni Rais wa wawamu yapili wa Tanzania ALLY HASSAN MWINYI ambaye ni Rais
mstaafu alikuja chuoni kwetu na kukubali yeye mwenyewe kuwa Chancellor wa chuo
chetu kama chuo chetu kinge kuwa hakitambuliki Rais mwinyi asingeweza kukubali
kuja chuoni kwetu kuongea nasi kwachuo ambacho hakitambuliki.’’aliongeza Mkurugenzi
wa masoko wa chuo hicho Thomas same.
KATIKA hatua
nyingine chuo hicho kimeanzisha progamu mpya ya masomo ya Bursal Scheme ambayo
inamuwezesha mwanafunzi aliyepo chuoni hapo kuweza kupata huduma za masomo kwa
punguzo la asilimia hamsini hususan kwa wanafunzi wakitanzania ambaye ana
ufaulu wakiwango chajuu .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni