Jumatatu, 16 Juni 2014

UNYANYASAJI WA WA WATOTO NCHINI WAWATISHIO

Timothy Marko
PAMOJA na jitihada mbalimbali zinazo fanywa na serikali katika kupunguza  vitendo vya unyaysasaji  kwa watoto nchini bado vitendo hivyo vimekuwa  vikishika kasi siku hadi siku  hali inyopelekea  kukwamisha maazimio yaliyowekwa na umoja wa afrika yakutaka nchi wanachama kunguza vitendo vya unyasasaji  wa  watoto ikiwemo ubakaji .
Akizungumza na waandishi wa habari jijini leo Kaimu Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC)Harod Sungusia amesema kuwa jamii imekuwa na dhana ya kubagua watoto hasa wenye ulemavu wa ngozi nawale wenyemtindio waubongo na wakimaumbilie .
‘’Kume kuwa na tabia katika jamii yetu Baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwaficha watoto nakuwanyanyapaa tumeweza kusikia habari mbalimbali kwenye vyombo vya habari tumekuwa tukishudia vitendo vya kikatili ambavyo vimekuwa vikifanywa nawazazi hususan katika mikoa ya kanda yaziwa na nyanda zajuu’’Alisema Harod Sungusia .
Harod sungusia alisema kuwa kumekuwa na visa vingi vya kubakwa na kulawitiwa kwa baadhi ya watoto vikishika kasi hapa nchini ambapo katika tafiti mbalimbali zilizofanywa na asasi mbalimbali imebainika kuwa watoto wengi wamekuwa wakifanyiwa vitendo hivyo vya ukatitili kutoka kwa wazazi wao walezi au jamaa wa karibu .
Aidha Kaimu mkurugezi wa kituo hicho Harod sungusia alisema kwamb a pamoja na kuwepo kwa sheria mbalimbali zinzo mlinda mtoto lakini kumekuwa navitendo vinavyokiuka haki ya mtoto .
‘’Matokeo yake kumekuwa namatukio mbalimbali yanayo muathiri mtoto ikiwemo mimba za utotoni magonjwa yazinaa ,ulemavu wa maisha wakati mwingine kuuwawa na nakujiua ‘’Aliongeza Kaimu Mkurugenzi.
Aliongeza kuwa hivi karibuni kumekuwa na habari mbalimbali kwenye vyombo vya habari vikiripoti kuhusiana namtoto aliyehifadhiwa kwenye boksi kwa takibani miakaminne nakusisitiza kuwa watoto wengi wamekuwa wakikatwa vidole nakuchomwa moto nakuunguzwa pasi.
Kaimu mkurugezi wakituo cha haki nasheria za binadamu Harod sungusia alisisitza kuwa jamii nyingi zimekuwa ziki kumbatia vitendo vinavyo mdhalisha mtoto.
‘’kumekuwa nakudharauliwa nakubaguliwa kwa mtoto ambapo jamii nyingi zimekuwa zikikumbatia dhana zinazo mkandamiza mtoto na kumuona mtoto siwakuthaminiwa kwa uzito wake’’Alisisiza.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni