Alhamisi, 12 Juni 2014

JESHI LA POLISI LA ENDELEA NA UCHUNGUZI KUHUSIANA NA CHANZO CHAMOTO SOKO LA MCHIKICHINI


Timothy Marko.
KUFUATIA  tukio la  moto mkubwa uliotokea jijini hivi karibuni,katika soko la mchikichini  jeshi lapolisi kaanda maalum jijini Dar es salam limesemakuwa bado linaendelea kufanya uchunguzi wa tukio hilo lili lo tokea jumatano majira ya saa tano usiku .

Akizungumza jijini jana na waandishiwahabari ,Kamishina wa jeshi  hilo lapolisi jijini Dares salaam suileiman kova alisema kuwa pamoja najuhudi zilizofanywa nakikosi cha  zimamoto na shirika la umeme Tanesco Moto huo ulikuwa niwenye kiwango kikubwa hali iliyopelekea kutekeza sehemu kubwa ya soko hilo lamchikichini kuteketezwa na moto.

‘’Jitahada zilifanywa nakikosi cha zimamoto kutoka jiji ,bandari na kampuni binafsi zenye magari yenye zimamoto hali ilikuwa ngumu sana kulingana na bidhaa zilizokuwa zinazoungua ikiwemo pamoja na nguo,viatu,mabegi pamoja navifaa vya plastiki ambavyo vilichochea moto kuweza kusambaa kwa kasi.’’Alisema Kamanda Suleiman Kova.

Kamanda Suileiman Kova alisema kuwa jeshi hilo liliweza kudhibiti vitendo vya kihalifu ambavyo ningeweza kutokea ambapo jeshi hilo lifanikiwa kudhibiti vitendo hivyo ambapo aliongeza kuwa lilifanikiwa kuzima moto majira saatisa usiku huku ulinzi ukimalishwa.

Alisema kufauatia tukio hilo lamoto hakuna alijeruhiwa wala kupoteza maisha nakuongeza kuwa mizigo iliyokuwemo katika  soko hilo haikuweza kuruhusiwa kuondolewa katika eneo la tukio  ilikuweza kupata uthibitisho wanahusika.

‘’Mpaka sasa haijaweza kufahamika chanzo cha moto huo kwakushirikiana na vikosi vyote vilivyotajwa awali uchunguzi bado unaendelea ilikuweza kujua chanzo halisi cha moto huo ikiwemo kwakutumia watalaam wakima abara ‘’alisema kamanda kova.

Katika hatua nyingine kamanda kova amesemakuwamnamo juni 10mwakahuko kawe  jeshi lake lilifanikiwa kukamata  bunduki moja aina ya SMG pamoja kiroba kilichukuwa kikisadikiwa kuwa nabangi nakufanikiwa kuwatia nguvuni watuhao .



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni