Mwenyekiti wa chama cha waajiri TanzaniaATE akizungumzia juu ya uhamasishaji wa waajiri kushiriki katika tuzo ya mwajiri bora wa mwaka (EYA) kwa mwaka 2013 |
Mwenyekiti wa chama cha waajiri Tanzania ATE ndugu Almas A. Maige ame wa hamasisha waajiri umuhimu wa kushiriki katika Tuzo ya mwajiri bora wa mwaka (EYA) 2013 Jijini Dar es Salaam
Amesema kuwa tunzo bora ya mwaka Employer of the year Award(EYA) ni tukio ambalo wamekuwa wakilifanya kila mwaka kwa mujibu wa kalenda ya chama Cha waajiri Tanzania(ATE) ambapo Tuzo hiyo imelenga
Kuwezesha uwepo wa namna bora kabisa ya kusimamia rasilimali watu,kitaalamu na kimazingira kwa nia ya kuleta tija na utendaji mahara pakazi
Pia moja ya shabaha ya tunzo bora ya mwaka ni pamoja na ; kutambua wanachama wa ATE ambao wameleta mifumo bora ya menejimenti ya rasiliimaliwatu kisera na kiutendaji, kutambua alama teule za waajiri kwenye usimamizi wa rasilimali, kutengeneza kanuni ambazo waajiri watazingatia ili kuboresha sekta ya rasilimaliwatu kwa kuwa na namna bora ya utendaji, kukusanya taarifa kuhusu rasilimali watu na kuangalia maeneo ambayo yanatakiwa kufanyiwa marekebisho ili kuyaboresha
Pia wanachama wote wa ATE wanakaribishwa kushiriki katika kinyanganyiro hicho bila kulipia ada
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni