Jumatatu, 6 Februari 2017

JESHI LAPOLISI LAMSHIKILIA MSANII WA BONGO MOVI .

Tokeo la picha la SIMONI SIRRO
KAMISHINA WA KANDA MAALUM DSM CP SIMONI SIRRO

Timothy Marko.
JESHI la polisi kanda maluum jijini Dar es salaam  linatarajia kumfikikisha Mahakamani Msanii wa maigizo Wema Sepetu Kesho baada ya kumuandikia hati ya Mashitaka yanayomkabili yakukutwa na misokoto ya bangi 104 na vifungashio vya misokoto baada ya kufanyiwa upelezi najeshi hilo.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Mapema hii leo Kamishina Simon Sirro amsema kuwa jeshi hilo liinamshikilia Msanii huyo wa Bongo MOVI sambamba na Mwenzake Omary Micheni (32)baada yawote hao kukiri kuhusika na tuhuma hizo .

''Baada ya kuwahoji mimi mwenyewe moja baada ya moja kukiri wazi walikuwa misikoto 104 sambamba 107 na baada ya kuhojiwa watuhumiwa hawa leo tuna waandikia hati ya mashitaka ili kesho waweze kupelekwa mahakamani ilikuweza kujibu tuhuma zinazo wakabili ''Alisema Kamishina wa Polisi Simon Sirro .

Kamishina sirro amesema jeshi hilo litahakikikisha haki inatendeka na halito mwonea mtu katika mapambano yakuteketeza mtandao wa madawa yakulevya katika jiji la Dar es salaam .
Alisema kuwa katika upelelezi uliofanywa najeshi hilo umebaini mtandao wa madawa yakulevya nimkubwa hivyo jeshi hilo linategemea kufanya operesheni kubwa juu ya madawa hayo huko Zanzibar .
''Tunawataka Wenyeviti waserikali za mitaa nchini kuweza kutoa taarifa juu yawatuhumiwa wanaohusika na madawa yakulevya ilikuweza kutokomeza mtandao huu wa madawa yakulevya nchini ''Aliongeza Sirro.

Katika hatua nyingine Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amesema kuwa vita ya madawa yakulevya siya jeshi hilo pekeyake bali ni lakila mtu anahusika katika vita hivyo .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni