MWENYEKITI WA BODI YA SHIRIKA LA POSTA Dk.HARUNI KONDO AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI MAPEMA HII LEO JIJINI DAR ES SALAAM. |
Timothy Marko.
SHIRIKA la Posta nchini limeiomba serikali kuweza kukamililisha madai ya fedha Takribani Bilioni nane malimbikizo ya gharama zake katika taasisi mbalimbali ilkuweza kujiendesha kibiashara .
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Mwenyekiti Wa Bodi ya shirika hilo Dk.Haruni Kondo amesema kuwa fedha hizo zinajumuisha fedha za taasisi za serikali nazile zisizo za kiserikali .
''Tuaiomba serikali pamoja na Taasisi zile za binafsi kuweza kukamilisha malipo ya majengo mbalimbali ,serikali tuinaidai shilingi bilioni 5.5 wakati Mashika nataasisi binafsi tunazidai shilingi bilioni 1.9 ''Alisema Dk. Haruni Kondo .
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Kondo amesema pamoja nakuidai serikali zaidi shilingi bilioni nane pia shirika hilo linatarajia kuwafikisha Katika vyombo vya sheria hilo waliobainika wanahihujumu shirika hilo kimapato .
Alisema shirika limeweza kufanya uchunguzi kumekuwa na wafanyakazi wa shirika hilo wamekuwa wakijihusisha navitendo vya ubadilifu ikiwemo matumizi mabaya yafedha za mafuta za magari za shirika hilo ambapo jumla ya shilingi bilioni 13 zimekuwa zititumiaka kulipia mafuta hewa katika shirika hilo .
''Tuanaitaka Menejimenti kuweza kuwabaini waliotumia shilingi bilioni 13 zilizotumika kulipia mafuta hewa kwa magari ambayo hadi hivi sasa hayajaonekana bado '' Aliongeza Dk. HARUNI KONDO .
Kondo Aliongeza kuwa anaitaka menejimenti ya shilika hilo kuweza kuwabaini wabadilifu wote waliweza kusababishia hasara shilika hilo kuweza kufukuzwa kazi .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni