Jumatatu, 10 Oktoba 2016

DSE:NGUVU YA SOKO YA ATHIRI MAUZO YAHISA DSE.



Timothy Marko
Hali yanguvu ya soko katika soko lahisa la Dar es salaam (DSE) katika kaunta ya kampuni yasigara nchini imeelezwa kuwa chanzo kikuu cha kupanda kwa mauzo yahisa katika soko la Dar es salam .

Akizungumza nawaandishi wahabari jijini Dar es salaam Afisa mwandamizi wa soko hilo Mary Kinabo amesema hali hiyo imechangia mauzo yahisa kuongezeka kwa asilimia65 kutoka shilingi bilioni 19.6 hadi kufikia shilingi bilioni 32.2 kwa wikihii .

''WAKATI takwimu zinaonesha idadi ya hisa zilizouzwa nakunuliwa imepanda zaidi yamara nne kutoka hisa milioni 2.4 hadi kufikia hisa milioni9 wakati huo huo makampuni yanayoongoza nipamoja na CRDB (70%) Ikifuatiwa kampuni yasigara ya TTC(25%) huku hisa za TBL zikiuzwa kwa asilimia 3%"Alisema Afisa Mwandamizi wa soko lahisa Mary Kinabo .

Afisa Mwandamizi Kinabo alisema kuwa wakati benki ya CRDB ikiongoza kuuza hisa zake  kwa asilimia sabini ukubwa wa mtaji wasoko umeshuka kwa asilimia 0.41 kutoka trilioni 21.576 hadi kufikia shilingi trioni 21.49 hali iliyochangiwa nakushuka kwa kaunta za NMG pamoja nakampuni ya ACA.

Alisema ukubwa wamakampuni yandani umepanda kwa asilimia0.35 kutoka trilioni 8.1 hadi trioni8.13 hali iliyochangiwa nakushuka kwa bei katika kaunta ya TBL .
''sekta yaviwanda imepanda kwapointi 26.16 baada ya hisa za TBL kupanda kwa asilimia 0.77 ikilinganishwa na kushuka kwa sekta yahuduma yakibenki kushuka 0.52 baada ya bei kushuka kwenye kaunta yaDSE kwa asimilia 1.54 ''Aliongeza kinabo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni