Mkurugenzi wa sensa ya watu na takwimu za jamii Ephraimu KWESIGABO akizungumza na waandishi(hawapo pichani )leo jijini DARES SALAAM. |
OFISI ya Takwimu nchini imesema kuwa Hali ya mfumuko wa bei kwa kipindi cha Mwezi agosti umepungua hadi kufikia 4.9 ikilinganishwa asilimia5.1 kwa mwezi julai mwaka huu
Akizungumza nawaandishi wahabari jijini Dar es salaam MKurugenzi wa sensa ya watu natakwimu za jamii nchini Ephraimu Kwesigabo amesema kuwa hali hiyo ya kupungua kwa bei za vyakula imetokana na upatikanaji wa bidhaa za vyakula sokoni .
''Kasi yaupandaji wabei za vyakula imeshuka hii ni kutokana na huduma za vyakula sokoni na kusababisha upatikanaji wabidhaa za vyakula kwa wingi sokoni ''Alisema Mkurugenzi wa Takwimu na sensa Ephraimu Kwesigabo.
Kwesigabo alisema kuwa wakati takwimu zikionesha mfumuko wabei kushuka kwa asilimia 4.9 fahirisi za bei zimeongezeka hadi 103.28 kutoka asilimia 98.49 kwakipindi cha mwezi Agosti mwaka huu .
Alisema Mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula navinywaji baridi kwa mwezi agosti umezidi kupungua na kufikia 7.0 kutoka asilimia 7.6 kwa kipindi cha mwezi julai mwaka huu .
''Kupungua kwa mfumuko wa bei kwakipindi cha mwezi agosti kumechangia kupungua kwa kasi ya upandaji wa bidhaa na zisizo za vyakula kwa kipindi kinachoishia mwezi agosti mwaka huu''Aliongeza KWESIGABO .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni