Jumatatu, 5 Septemba 2016

DSE : KUMEKUWA NAMWITIKIO MKUBWA KWA WANAFUNZI WA ELIMU YAJUU KATIKA KUWEKEZA .

Tokeo la picha la mususa

Meneja  Mauzo na Biashara DSE Patrick MUSUSA



Timothy Marko.
IDADI  ya  mauzo ya hisa katika soko  la Dar es salaam Stock Exchange (DSE) imeongezeka  kwa asilimia 75 kutoka shilingi bilioni 2.2 hadi kufikia bilioni 3.8 huku ikiwa mtaji wa makampuni ya ndani umeshuka kwa asilimia 8.5 kutoka trioni 20 hadi kufikia trioni 20.8 kwa wiki iliyopita .

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Menejamiradi Masoko na Biashara Patrick Mususa amesema kuwa Hali hiyo imechangiwa na shughuli mabalimbali za manunuzi na kuuza hisa zao baada ya soko hilo kukuza uelewa ikiwemo kutumia vyombo vya habari juu yaumuhimu wa hisa katika kukuza uchumi .

‘’Wakati huo huo Makapuni yanayo ongoza katika kuuza hisa katika soko lahisa nipamoja CRDB kwa asilimia 28 ,DSE Asilimia 22 huku kampuni ya sigara nchini ya TCC ikishika nafasi yatatu kwa asilimia 21 kwa kwa kununuliwa hisa zake ‘’Alisema Meneja Miradi na Biashara Patrick Mususa .
Mususa alisema kuwa wakati mauzo ya hisa yaikiongezeka kwa asilimia 75 sekta ya viwanda imeshuka kutokana na kupungua kwa kaunta ya kampuni ya bia nchini (TBL) kwa asilimia 2.6 

Alisema kuwa Sekta yakibenki imeonekana kushuka kutokana na ongezeko lahisa katika kaunta ya soko lahisa kushuka kwa asilimia 0.82 

‘’Sambamba na hilo pia katika soko letu kumekuwa na mwitikio mkubwa kwa wanafunzi hasa katika kipindi cha mwaka jana ambapo wanafunzi wengi walijitokeza kununua hisa kwa asilimia 50 ikilinganishwa na mwaka huu ambapo mkoa wa Arusha ndio umekwa ukiongoza kwa wanafunzi kuwekeza kupitia soko la Hisa ‘’ Aliongeza Mususa .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni