BAADHI YA MABEHEWA YA SHIRIKA LA RELI YANAYO TUMIKA KATIKA USAFIRI KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM. |
Timothy
Marko.
KATIKA kuhakikisha sekta ya usafirishaji inaimarika shirika
la reli nchini (TRL) imetoa nauli elekezi ya shilingi 600 kwa wasafiri wanaotumia
usafiri wa reli kwa wakaazi jiji la Dar
es salaam.
Akizungumza
na waandishi wahabari jijini Dar es salaam Kaimu Mkurugenzi wa shirilika hilo
Nghwani Mdema amesema kuwa nauli hiyo elekezi ya shilingi 600 itaanza kutozwa
baada ya wiki mbili kuanzia leo .
‘’Nauli hii
itaendana sambamba na ile ya wanafunzi 100 baada ya mamlaka ya usafirishaji
majini nan chi kavu kufanya ukokotozi juu ya gharama ya nauli ya usafiri huu ‘’Alisema
Kaimu Mkurugenzi Ngwani Mdema .
Kaimu
Mkurugenzi Mdema alisema kuwa katika kuboresha huduma ya shirika la Reli
shirika hilo linatarajia kuongeza mabehewa mawili ambapo hapo awali shirika
hilo lilikuwa likitumia mahewa kumi nane na kufikikia mabehewa ishirini.
Alisema
wa agosti 9 mwaka huu waziri wa ujenzi
,uchukuzi na mawasiliano Profesa Makame Mbarawa alizindua safari za kutoka
katikatikati ya jiji la Dar es salaam kwenda pugu huku shirika hilo likiwa na
mabehewa 15 yanayotumika kusafirisha abiria .
‘’Kwa
kipindi cha wiki moja shilika hili likuwa likitoa huduma kwa wananchi na
wakaazi wa Dar es salaam awamu mbili asubuhi na jioni bila kutoza malipo yeyote’’Aliongeza
Mdema .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni