MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM PAUL MAKONDA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI. |
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewataka Wafanyabiashara wadogo wadogo kutotumia vituo vya mabasi vya mwendokasi kama sehemu ya vyoo nakujisitiri na baadalayake kuayaacha maeneo hayo kama yalivyokusudiwa .
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mkuu huyo wa Dar es salaam amesema kuwa hivi karibuni amepata malalamiko kutoka katika uongozi wa mradi wamabasi yaendayo haraka DART kuwa kumekuwa na wafanyabiashara wadogo wadogo huyatumia maeneo yaliyotengwa na mabasi hayo kama vituo kama vyoo.
''Hivi karibuni nimepokea malalamiko kutoka kwenye uongozi wa DART ya kuwa kumekuwa na baadhi ya wafanyabishara wadogowadogo wakitumia vituo hivi vya mabasi yaendayoharaka maarufu DART kama sehemu ya vyoo''Alisema Mkuu wa mkoa Paul Makonda .
Makonda alisema kuwa kutokana hali hiyo iliyojitokeza amewataka wafanyabishara kutoingilia maeneo hayo kwaminadi ya kufanyabishara na badalayake kuyaacha maeneo hayo yatumike kama ilivyokusudiwa .
Alisema nilazima wafanyabishara hao kufuata utaratibu namisingi ya sheria ikiwemo kuzingatia kanuni za usafi wamazingira na kufuata kanuni za mipango miji kama ilivyokusudiwa .
''Hakuna haki pasipo kutenda haki hivyo ninawataka wafanyabishara kuzingatia kanuni za usafi kwani hivi karubuni tunao mpango wakujenga miundombinu ikiwemo ya vyoo katika vituo vya mwendokasi ''Aliongeza Mkuu wa mkoa Paul Makonda.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni