Afisa Mwandamizi wa Soko la hisa la Dar es salaam (DSE)Mary Kinabo |
Afisa Mwandamizi wa Soko la hisa la Dar es salaam (DSE)Mary Kinabo amesema kuwa hali ya kushuka kwa mauzo yahisa katika kipindi cha wiki iliyopita imechangiwa na sikuu ya nane nane ambayo huadhimishwa kila Agost 8 ya kila mwaka .
Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar es salaam Mary Kinabo amesema kuwa katika takwimu za soko hilo zimeonesha kuwa idadi yamauzo yahisa yalishuka kwa asilimia 81 kutoka shilingi bilioni11.3 nakuweza kufikia shilingi bilioni 2.1
''Wakati hali hiyo ikitokea benki ya CRDB ilikuwa ikiongoza kwa asilimia 38.08 ikifuatiwa Soko la hisa la Dar es salaam kwa asilimia 27.55 huku Benki ya NMB Ilishika na nafasi yatatu kwakuuza hisa zake kwa asilimia 22.94 ''Alisema Afisa Mwandamizi wasoko la hisa Mary Kinabo .
Afisa Mwandamizi Mary Kinabo alisema kuwa wakati benki ya CRDB ikiongoza kwa kununuliwa hisa zake kwa asilimia 38.08 ukubwa wa mtaji wa soko umeshuka kwa asilimia 5.73 nakufikia shilingi trioni 24.6 kutoka trioni 23.2
Alisema kuwa wakati ukubwa wamtaji wasoko ukishuka kwa asilimia5.73 ukubwa wamtaji wa makapuni yandani umepanda kwa 0.88 asilimia na kufikia shilingi 8.4 trioni .
''SEKTA yaviwanda kwa wiki hii imeonesha kushuka kwa pointi 5.1 baada ya hisa za TOL kushuka kwa asilimia 6.25 wakati TBL kwa asilimia 0.07 hata hivyo sekta yakibenki imepanda baada hisa za kaunta ya DSE kupanda kwa aslimia 20 wakati NMB ikishika Asilimia 5.86 ''Aliongeza Mary .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni