Jumanne, 14 Juni 2016

WAZIRI NDALICHAKO AWATAKA KUMSAIDIA KATIKA KUBORESHA SEKTA YA ELIMU NCHINI.

Tokeo la picha la ndalichako
waziri waelimu namafunzo yaufundi Profesa JOYCE NDALICHAKO.


Timothy Marko.
SERIKALI imesema kuwa katika kuhakikisha sekta ya elimu inakuwa natija hapa nchini itaendelea kushirikiana nawadau mbalimbali wasekta hiyo ikiwemo jamii ili kuwezesha mpango wezeshi unaolenga kukuza kiwango cha ubora wasekta hiyo .

Akizungumza katika kongamano la uzinduzi wa ripoti ya ubora waelimu unaolenga kutathimini Kusoma kuandika na kuhesabu Waziri wa Elimu na mafunzo yaufundi Profesa Joyce Ndalichako amesema kuwa ilikuwezesha mpango wa uboreshwaji wa sekta ya elimu nilazima wadau mbalimbali wakiwemo wazazi walimu watunga mitaala yaelimu kuweza kushirikiana katika kuwezesha mpango wa KKK una tekelezwa kwa vitendo .

‘’Tunahitaji matokeo bora katika kuhakikisha mpango huu wa KKK yani kusoma kuandika nakuhesabu unatekelezwa kwa vitendo  kama hatutashirikiana na wadau mbalimbali wasekta yaelimu KKK hazitoweza kukamilika ‘’Alisema Profesa Joyce Ndalichako .

Waziri wa elimu na mafunzo yaufundi profesa Ndalichako alisema kuwa katika kuwezesha mpango huo wa kujua kusoma kuhesabu na kuandika unatekelezwa serikali itashirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo wadau mbalimbali wa mandeleo ikiwemo shirika la USAID ilikuweza kuhakikisha mpango huo wa ubora waelimu wa kujua kusoma kuhesabu nakuandika unatekelezwa .

‘’Katika kulifanikisha hili la ubora waelimu naiomba jamii isiachwe nyuma katika kuboresha sekta ya elimu ikiwemo kuweka mipango mikakati ya kuboresha sekta ya elimu ikiwemo kuboresha mazingira wezeshi ya zana zakufundishia ikiwemo madarasa vitabu pamoja na ubora wa walimu ‘’Aliongeza Waziri waelimu na mafunzo yaufundi profesa Joyce Ndalichako.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni